UTANGULIZI
Watu wengi wamekuwa wakitumia nguvu za Mungu vibaya au wakipungukiwa haraka nguvu za Mungu kutokana na kutofahamu ufunuo wa kutunza nguvu hizo au kupuuzia ufunuo waliopewa na Mungu kuhusu namna ya kutunza nguvu hizo.
Kwa mfano watu ambao wamewahi kutumia dawa fulani kutoka Kwa waganga wa kienyeji wanafahamu kuwa kuna dawa zingine ukipewa zinakuwa na masharti kwamba usile mboga za majani au usisalimiane na watu Kwa kupeana mikono au ukitoka au kuingia ndani uanze kuingia kwa mguu wa kushoto nakadhalika.
Masharti hayo yanakuwa na lengo la kutunza nguvu hizo ziendelee kutenda kazi ndani ya mtu.
Ndivyo ilivyo pia nguvu za Mungu kama hauna ufunuo wa kuzitunza ili ziendelee kutenda kazi ndani yako utajikuta unaishiwa haraka nguvu za Mungu.
TAZAMA MIFAMO HII
✓ SAMSONI (Waamuzi 13:2-5)
Samsoni alipewa ufunuo wa kutunza nguvu za Mungu ndani yake, aliambiwa "asinyoe nywele"
Siku Samsoni aliyonyolewa nywele ndio siku ambayo zile nguvu zilizokuwa zinatenda kazi ndani yake zilitoweka (Waamuzi 16:18-19)
✓ BWANA YESU (Mathayo 4:1-4)
Ibilisi alimwambia Yesu ukiwa ndiwe mwana wa Mungu "amuru kwamba mawe haya yawe mikate"
Ibilisi alichokuwa anawinda ni nguvu zilizoko ndani ya Yesu, Ibilisi alijua kuna nguvu ambazo Yesu amezipata kupitia mfungu wa siku 40 Kwa hiyo akatamani kuhakikisha hizo nguvu zinatoweka ndani ya Yesu.
Nguvu za kubadili mawe kuwa mikate zilikuwa ndani ya Yesu lakini hakubadili yale mawe Kwa sababu
Kama angeyabadili mawe kuwa mikate angekuwa amemtii shetani.
Kuna nguvu zingemtoka zikabadili yale mawe kuwa mikate.
Yesu alipata ufunuo wa kutumia neno la Mungu kumpinga Ibilisi.
HITIMISHO
✓ Kama hauna ufunuo wa kutunza nguvu za Mungu, omba Mungu akupe ufunuo wa kutunza nguvu zake ndani yako.
✓ Kama una ufunuo zingatia Sana ufunuo huo, Samsoni alipoacha kuzingatia ufunuo aliopewa nguvu zilimtoka akabaki mtu wa kawaida hatimaye wafilisti walimuweza wakamtoboa macho pia wakamtumikisha.
0 Maoni