ANAJIBU KWA UTUKUFU WAKE ANANYAMAZA KWA UTUKUFU WAKE


 Faraja Gasto ✍️✍️✍️✍️

(Yohana 11:1-44)

Yesu alikuwa anampenda Lazaro lakini alipoitwa kumponya HAKWENDA.

Lazaro alipokufa ndipo Yesu akaenda (Yesu hakwenda msibani bali kumfufua).

Ndugu zake Lazaro walikuwa na haraka ya kuona uponyaji wa ndugu yao lakini YESU HAKUWA NA HARAKA YA KUMPONYA.

SABABU YA KUKUKUMBUSHA KISA HICHO

Nimekukumbusha kisa hicho ili kukutia moyo, kuna wakati unaweza ukapitia kipindi kigumu sana ukamuita Yesu lakini HAUONI MAJIBU YOYOTE.

Unapaswa kukumbuka kuwa pamoja na yote unayopitia YESU BADO ANAKUPENDA SANA.

Yamkini ukajiuliza kama ananipenda Sana mbona haniitikii?

Kumbuka kisa cha Lazaro, Yesu aliitwa kuponya lakini hakuja japo alikuwa anampenda Lazaro ila Lazaro alipokufa ndipo Yesu akaja, YESU HAKUWA NA HARAKA YA KUMPONYA LAZARO ILA ALITAKA KUMFUFUA ILI MUNGU APATE UTUKUFU MKUBWA ZAIDI.

Kwa hiyo kama Yesu amenyamaza hakuitikii usidhani hakupendi, ANAKUPENDA SANA ILA KUNA WAKATI ANANYAMAZA KWA AJILI YA UTUKUFU WAKE.

NB: Anajibu kwa ajili ya utukufu wake pia ananyamaza kwa ajili ya utukufu wake.


Chapisha Maoni

0 Maoni