Faraja Gasto ✍️✍️✍️
Kuna msemo usemao "fikiri kabla ya kutenda" ni msemo wa kawaida lakini umebeba hekima kubwa ndani yake.
Watu wengi tunapotenda mambo mbalimbali huwa hatufikiri kesho au matokeo ya jambo hilo baada ya kulitenda.
Tuko katika zama za kidijitali, katika zama ambazo matumizi ya mitandao ya kijamii yamekua kwa kiwango kikubwa sana kiasi kwamba wapo baadhi ya watu wasipotumia mojawapo ya mitandao ya kijamii kwa siku moja wanajihisi kama wamepungukiwa kitu kikubwa maishani mwao hatimaye wengine huamua kukopa fedha, kutumia simu za wengine au tarakilishi za wengine ili wajue nini kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii.
Bahati mbaya sana wapo watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kuchapisha picha au video ambazo zinaunga mkono harakati za mmomonyoko wa maadili (picha au video za utupu, ngono n.k) wapo baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuongea mambo ya kipumbavu n.k
NATAKA UFAHAMU KUWA
Kama haujui kesho na keshokutwa utakuwa nani epuka sana kutumia mitandao ya kijamii kuchapisha picha na video ambazo zinaunga mkono harakati za mmomonyoko wa maadili pia epuka kuongea mambo ya kipuuzi.
Kama una maono ya kuwa mtu unayeheshimika katika jamii epuka sana kutumia mitandao ya kijamii kufanya mambo ya kihuni, kuongea mambo ya kipumbavu n.k
NB:
✓ Sisi tunaweza kusahau haya mambo ya kwenye mitandao lakini mitandao yenyewe haisahau, ipo siku itatukumbusha mambo yako, ITUMIE VIZURI.
✓Laiti kama Mheshimiwa Jokate Mwegelo na wengineo wangejua watakuja kuwa na nafasi walizonazo leo naamini kuna picha ambazo wangeepuka kuzipiga, kuna video wangeziepuka ili sura zao zisionekane kwenye video hizo.
Ni mimi wako,
Faraja Gasto.
0 Maoni