DUNIA KAMA CHUMBA CHA MITIHANI


✍️Faraja Gasto

Dunia ni kama chumba cha mtihani, kila mwanadamu ni mtahiniwa au mtu ambaye anapaswa kufanya mitihani mbalimbali.

Baada ya kumaliza kufanya mitihani watu husitisha masomo kwa muda au kuhitimu masomo.

Mwalimu ndiye hakimu ambaye anaamua nani kafanya vizuri au nani kafanya vibaya, wanaofanya vizuri huwa wanafaulu na waliofanya vibaya huwa wameshindwa hatimaye hurudia masomo nakadhalika.

IKO HIVI

KUFA ni kama kutoka kwenye chumba cha mtihani.

Mungu ni kama mwalimu anayehukumu nani kafanya vizuri au vibaya.

Wote waliofanya vibaya au walioshindwa kufanya vizuri kwenye mtihani (waliomkataa Yesu) wametengewa eneo lao maalumu linaitwa JEHANAMU.

Wote waliofanya vizuri (waliomwamini Yesu na kuishi sawasawa na matakwa yake) wametengewa eneo lao maalumu linaitwa MBINGUNI.

SWALI

Je! baada ya kumaliza mitihani ya hapa Duniani utakwenda wapi? Mbinguni au Jehanamu.

NAMNA YA KUFAULU 

Ni kumpa Yesu maisha yako na kuishi sawasawa na inavyokupasa kuishi kama kiumbe kipya (Yohana 1:12)(1 Yohana 2:6)

KUMBUKA

“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;”

   Waebrania 9:27 


Yohana 3 

¹⁶ Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

¹⁷ Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

¹⁸ Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.


Chapisha Maoni

0 Maoni