✍️Faraja Gasto
Mungu huwa anapeleka watu mbele kwa ajili ya wengine, kwa mfano Mungu alimpeleka mbele Yusufu kwa ajili ya ndugu zake (Mwanzo 45:5)
Mungu alimtanguliza Yohana Mbatizaji kwa ajili ya Yesu (Mathayo 3:11)
NB: Watu hao Mungu huwasaidia kupata nafasi fulani, aina fulani ya maisha nakadhalika kwa ajili ya watu wengine.
Pia shetani huwa anapeleka watu mbele ili kuharibu maisha ya wengine, kwa mfano shetani alimsaidia Hamani Bin Hamedatha kupandishwa cheo ili kuwaangamiza wayahudi (Esta 3:1,5&6)
NB: Shetani huwasaidia watu hao kupata nafasi fulani, aina fulani ya maisha nakadhalika ili kuharibu au kuwaangamiza watu wengine.
USISAHAU
Kumuomba Mungu awaondoe watu ambao shetani amewatanguliza mbele ili kuharibu maisha yako.
0 Maoni