UTANGULIZI
Mungu huwapa watu maelekezo mbalimbali na kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya ndoto, maono, ushauri nakadhalika.
Yapo mambo mbalimbali ya kufanya ili upate maelekezo kutoka kwa Mungu, baadhi ya mambo hayo ni maombi na kutoa sadaka.
Katika makala hii nataka tutazame mifano ya watu mbalimbali waliopokea maelekezo ya Mungu baada ya kutoa sadaka.
MIFANO YA WATU WALIOPATA MAELEKEZO YA MUNGU BAADA YA KUTOA SADAKA
MFANO WA 1: MZEE YETHRO (BABA MKWE WA MUSA)
(Kutoka 18:12-27)
Siku iliyofuata baada ya baba mkwe wa Musa kumtolea Mungu matoleo, alimuona Musa akiendelea kutekeleza majukumu yake, ghafla katika moyo wa mzee Yethro kuliingia maelekezo ya kumpa Musa ili afanye kazi kwa ufanisi.
Ile sadaka ilipelekea Musa kupata maelekezo ya kumsaidia katika utumishi wake.
MFANO WA 2: MAMA JUSI WA MASHARIKI
(Mathayo 2:11-12)
Mamajusi wa mashariki walipomuona Yesu walimtolea tunu, uvumba, dhahabu na manemane, walipolala Mungu aliwapa maelekezo kwa njia ya ndoto wasirudi Kwa Herode.
Tunu, dhahabu, uvumba na manemane yalikuwa ni matoleo waliyomtolea Yesu.
MFANO WA TATU: KORNELIO
(Matendo ya mitume 10:1- 48)
Malaika alipomtokea Kornelio alimwambia "Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho"
Baada ya kuambiwa maneno hayo akapewa maelekezo yaliyopelekea akaokoka yeye na watu wengi.
HITIMISHO
Hiyo ni baadhi ya mifano ya watu ambao waliopokea maelekezo ya Mungu kupitia sadaka walizotoa.
Hivyo basi fahamu sadaka inaweza ikakufungulia mlango wa kupata maelekezo ya Mungu ya kukusaidia wewe na kuwasaidia wengine.
Unahitaji maelekezo gani kutoka kwa Mungu? baadhi ya njia zitakazokusaidia kupata maelekezo hayo ni maombi, kama umeomba na haujapata maelekezo jifunze kumtolea Mungu sadaka.
0 Maoni