BAADHI YA WAJIBU WA MKRISTO KATIKA UFALME WA MUNGU


 ✍️Faraja Gasto


UTANGULIZI

Kila raia wa nchi husika ana haki zake kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo pia ana wajibu ambao anaopaswa kuutimiza yeye kama mwananchi.


Vivyo hivyo kila aliyemwamini Yesu na kumkiri kuwa ni Bwana ni raia wa mbinguni (Waefeso 3:20)


Kwa kuwa kila mwamini ni raia wa mbinguni anao wajibu wa aina mbalimbali anaopaswa kuutimiza kwa ajili ya ufalme wa Mungu (Wakolosai 1:10)


WAJIBU WA MWAMINI


✓KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE BILA KUJALI MADHEHEBU YAO, NCHI ZAO ZA HAPA DUNIANI NAKADHALIKA

(Waefeso 6:18)


Kila mmoja ana wajibu wa kuwaombea wengine bila kujali madhehebu yao, nchi nakadhalika.


✓KUMPENDEZA MUNGU


(Wakolosai 1:10)

Kila mwamini anapaswa kumpendeza Mungu (kufanya yanayomfurahisha Mungu).


Ili tuweze kumpendeza Mungu lazima tuamini kwa kuwa pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6) kwa maana nyingine ni kwamba hatuwezi kumpendeza Mungu bila kuwa na neno la Mungu mioyoni mwetu, inakuja kwa kusikia neno la Kristo (Warumi 10:17).


Yesu alipokuwa hapa duniani alimpendeza Mungu mpaka Mungu akashuhudia kwamba Yesu ni mwanaye mpendwa anayependezwa naye (Mathayo 3:16-17)(Luka 2:52)


✓KUMZALIA MUNGU MATUNDA KWA KILA KAZI NJEMA 


(Wakolosai 1:10)


Zipo kazi mbalimbali tunazoweza kuzifanya na zikamzalia Mungu matunda kwa mfano kushuhudia au kuhubiri injili, kufanya maombezi nakadhalika.


Kila mwamini anapaswa kuwa na kazi ambayo au ambazo anafanya kwa ajili ya ufalme wa Mungu kwa kuwa Kila mtu atapewa thawabu kulingana na kazi ambazo anazifanya (Ufunuo wa Yohana 22:12)



HITIMISHO

Kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake katika ufalme wa Mungu kwa kuwa Mungu anatutaka tutimize wajibu wetu (Wakolosai 1:10)

Chapisha Maoni

0 Maoni