✍️Faraja Gasto
UTANGULIZI
Mungu muumbaji ana sifa nyingi sifa mojawapo aliyonayo ni kuaminiwa (2 Timotheo 2:13) hata kama wengine hawamuamini haimfanyi yeye kutokuaminika.
Mungu huwapa watu neema mbalimbali, neema mojawapo ambayo Mungu huwapa watu ni "neema ya kuaminika au neema ya kuaminiwa" mtu akiwa na neema hii anakuwa anaaminika kirahisi sana, mtu atajikuta anaaminika, anaweza kupewa mali, fedha nakadhalika sio kwa sababu ya elimu au ujuzi bali ni kwa sababu anaaminika.
MIFANO YA WATU AMBAO MUNGU ALIWAPA NEEMA YA KUAMINIWA
✓ YUSUFU
(Mwanzo 39:4-6)
Mungu alimpa Yusufu neema ya kuaminiwa, neema hii ilisababisha Yusufu akawa meneja wa miradi na mali za Potifa.
Potifa alijikuta anamuamini Yusufu japo hajui historia yake, japo Yusufu hakuwa na elimu rasmi ya usimamizi wa rasilimali lakini Potifa akajikuta anamuamini na kumkabidhi rasilimali zake azisimamie.
✓DAUDI
(1 Samweli 18:4-5)
Neem ya kuaminiwa ilikuwa juu ya Daudi, neema hii ilimfanya Daudi kuaminiwa na Mfalme Sauli akapewa kazi mbalimbali.
Neema hii ilimfanya Daudi akapewa cheo cha ukuu wa Jeshi la Sauli, Daudi ambaye hakuwahi kuwa askari akapewa cheo cha kuwa mkuu wa Jeshi la Sauli na watu wote wakakubaliana na maamuzi ya Mfalme Sauli.
Jaribu kufikiri mtu wa kawaida ambaye sio askari anapewa cheo kuwa mkuu wa Jeshi halafu wanajeshi hawapingi usidhani ni jambo la kawaida, ni neema ilihusika kusababisha jambo lile litokee.
BAADHI YA MBINU ZA KUTUNZA NA KUONGEZA NEEMA YA KUAMINIWA
✓UWE MWAMINIFU
Zifuatazo ni baadhi ya maana za uaminifu. Uaminifu ni kutokwenda kinyume na mapatano au makubaliano, uaminifu ni kutenda sawasawa na maelekezo au maagizo, uaminifu ni kutimiza ulichoahidi.
(Mwanzo 39:7-10)
Yusufu aliambiwa na Potifa kuwa asimamie vitu vyote ila awe mbali na mke wa Potifa, Yusufu alikuwa mwaminifu ndio maana mke wa Potifa alipomtamani Yusufu akataka alale naye kimapenzi, Yusufu alikataa kwa kuwa aliambiwa akae mbali na mke wa Potifa.
Yusufu alidumu katika uaminifu hatimaye Mungu alimpa cheo kikubwa zaidi ya alichokuwa nacho kwa Potifa (Mwanzo 41:39-41)
(Mathayo 25:14-28)
Wale watumwa waliaminiwa wakapewa fedha ili wazalishe lakini mmoja wao hakuzalisha, wale waluozalisha fedha waliitwa watumwa Wema na waaminifu hatimaye wakapewa mamlaka zaidi lakini yule ambaye hakuzalisha aliitwa mtumwa mbaya na mlegevu akanyang'anywa fedha aliyokuwa nayo kwa kuwa alikosa uaminifu.
NB: Mungu akikupa neema ya kuaminiwa hakikisha unakuwa mwaminifu, ukipewa kazi fanya kazi kwa bidii, ukipewa maelekezo tekeleza sawasawa na ulivyoelekezwa, ukitoa ahadi hakikisha unatimiza ahadi hiyo, ukikopa hakikisha unalipa, ukifanya hivyo utazidi kuaminika au kuaminiwa.
✓ UWE MNYENYEKEVU
(1 Petro 5:5-6)
Unyenyekevu hufungulia neema kuja kwenye maisha ya mtu pia unyenyekevu huongeza neema zaidi.
UMUHIMU WA NEEMA YA KUAMINIWA
✓Inakufanya uaminike kirahisi sana.
✓Inakufanya upate nafasi, kazi nakadhalika.
0 Maoni