UKAGUZI KABLA YA SAFARI


 ✍️ Faraja Gasto


UTANGULIZI: USHUHUDA


Watu watano walisafiri kwenda mkoa mwingine kwa ajili ya kushiriki harusi, wakati wakiwa njiani wakakuta maaskari wa idara ya uhamiaji wakifanya ukaguzi, walipokaguliwa mmoja wao akakutwa na kitambulisho bandia hivyo basi wote watano wakakamatwa kwa kuwa walikuwa pamoja.


Kutokana na kile kitambulisho bandia alichokutwa nacho mmoja wao wakatafsiriwa kuwa wanafanya biashara haramu ndio maana wana kitambulisho bandia.


Kwa hiyo mtu mmoja aliwaponza wote.


MIFANO YA BIBLIA INAYOTUSAIDIA KUFAHAMU UMUHIMU WA UKAGUZI KABLA YA SAFARI


MFANO WA 1: SAFARI YA KUELEKEA TARSHISHI 


(Yona 1:1-15)

Mungu alimtuma Yona kwenda Ninawi lakini Yona akaamua kwenda Tarshishi, wakati wakiwa safarini Mungu akatuma upepo mkali wakaanza kutaabika wakatupa shehena kwenye maji ili wajiokoe lakini hali ilizidi kuwa mbaya.


Hatimaye wakaamua kufanya ukaguzi wajue mabaya yale yaliwapata kwa sababu ya nani, hatimaye wakagundua ni Yona.


Yona aliwaponza wenzie pia aliwasababishia hasara wenzie.


Laiti kama wangekaguana mapema wasingepata hasara ile.


MFANO WA 2: SAFARI YA YAKOBO NA FAMILIA YAKE WAKATI WA KUTOKA KWA LABANI


(Mwanzo 31:22-34)

Raheli aliiba miungu ya baba yake akaificha bila Yakobo na wengine kufahamu hilo, jambo hilo lilisababisha Labani akakasirika zaidi akaamua kuanza kuwafuatilia kwa lengo la kuwatenda mabaya Yakobo na watu aliokuwa nao, kama Mungu asingeingilia kati basi Labani angewafanyia mabaya maana alikusudia mabaya (Mwanzo 31:24,29)


Laiti kama Yakobo angefanya ukaguzi kabla ya safari angeepuka kufuatiliwa na Labani.


BAADHI YA FAIDA ZA  KUFANYA UKAGUZI KABLA YA SAFARI


✓Ukaguzi unasaidia kubaini vitu vinavyoweza kusababisha hatari katika safari.


✓Ukaguzi unasaidia kutokusahau vitu ambavyo ni vya muhimu kuwa navyo katika safari (vitambulisho, mavazi, vifaa nakadhalika)




Chapisha Maoni

0 Maoni