UTANGULIZI
Katika kuishi kwetu duniani tunapaswa kuishi huku tukijitambua
✓Sisi ni akina nani
✓Wapi tulitoka
✓Wapi tunakwenda
✓Wajibu wetu ni nini
✓Tukoje (madhaifu yetu, uwezo wetu nakadhalika)
Kujitambua kutatusaidia mambo mengi na kutatunufaisha sana.
Kujitambua ni hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye mafanikio ya aina mbalimbali.
BAADHI YA FAIDA ZA KUJITAMBUA
✓KUTAKUSAIDIA KUJUA KIPI KINAKUPASA UFANYE NA KIPI HAUPASWI KUFANYA.
(Mwanzo 39:1-10)
Yusufu aliponunuliwa na Potifa, Potifa alimpangia majukumu mbalimbali, wakati akiendelea na majukumu yake, mke wa Potifa akamtaka Yusufu kimapenzi lakini Yusufu alikataa.
Yusufu alikataa kwa kuwa alikuwa anatambua kuwa majukumu yake ni mengine, hakupewa jukumu la kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa Potifa.
NB: Kuna mambo yatakuwa mepesi kuyafanya endapo utajitambua wewe ni nani pia Kuna mambo utaepuka kuyafanya ukijitambua wewe ni nani.
✓KUJITAMBUA KUTAKUSAIDIA KUTIMIZA MALENGO YAKO
(Luka 19:1-10)
Zakayo alikuwa na lengo la kumwona Yesu lakini hakufanikiwa kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo pia umati wa watu ulimzuia kumwona Yesu.
Zakayo alipojitambua mimi ni mfupi alimua kupanda juu ya mti uitwao mkuyu, alipopanda juu ya mti alimwona Yesu.
✓KUJITAMBUA KUTAKUSAIDIA KUBADILISHA MAISHA YAKO AU KUBORESHA MAISHA YAKO
(Luka 15:11-24)
Huyu kijana alipewa mali akazitumia vibaya hatimaye akawa masikini, alipojitambua kuwa yeye ni mtoto wa tajiri aliamua kurudi Kwa baba yake, aliporudi kwa baba yake maisha yake yalibadilika kabisa akaondokana na umasikini uliokuwa umempata.
HITIMISHO
Kama wewe ni mtoto tambua kuna wajibu wako kama mtoto pia kuna mambo hupaswi kufanya, kama wewe ni mume wa mtu kuna wajibu wako wa kuutimiza pia kuna mambo hupaswi kufanya, kama wewe ni mke wa mtu kuna wajibu wako wa kuutimiza pia kuna mambo hupaswi kufanya.
Kama wewe ni mtumishi wa Mungu kuna wajibu wako wa kuutimiza pia kuna mambo hupaswi kufanya, kama wewe ni mwajiri kuna wajibu wako wa kuutimiza pia kuna mambo hupaswi kufanya, kama wewe ni mwajiriwa kuna wajibu wako wa kuutimiza pia kuna mambo hupaswi kufanya.
Kujitambua kutakusaidia mambo mengi sana ikiwemo kujua yanayokupasa kufanya na mambo ambayo hupaswi kufanya, kujitambua kutakusaidia kubadilisha maisha yako pia kutakusaidia kutimiza malengo yako.
0 Maoni