✍️Faraja Gasto
(Mathayo 7:7)
UTANGULIZI
Kufuatana na Mathayo 7:7 tunaona Mungu anasema tukiomba kwake tutapewa kile tulichoomba.
Mungu hujibu maombi kwa njia mbalimbali ikiwemo KUPITIA UFUNUO AU KUMPA MTU UFUNUO AU KUMFUNULIA MTU JAMBO FULANI.
Mungu huwapa watu ufunuo ili kupitia ufunuo ule wapate majibu wa maombi yao waliyomuomba.
Unaweza kujiuliza ufunuo ni nini?
✓Ufunuo ni maelekezo maalumu ambayo Mungu humpa mtu.
✓Ufunuo ni siri ambayo Mungu humfunulia mtu.
MIFANO YA KIBIBLIA INAYOONYESHA NAMNA MUNGU ANAJIBU MAOMBI KUPITIA UFUNUO
MFANO WA 1: UFUNUO ALIOPEWA MWANAMKE ALIYETAKA KULIPA DENI
(2 Wafalme 4:1-7)
Mume alikufa akaacha deni, aliyekuwa anadai akaja kuchukua watoto ili wawe watumwa kufidia lile deni.
Huyu mwanamke alimwendea Nabii Elisha akamueleza, wakati huohuo Nabii Elisha akapata ufunuo wa kumpa yule mwanamke.
Yule mwanamke alipozingatia ule ufunuo alipata pesa ya kulipa deni na ziada.
MFANO WA 2: UFUNUO WALIOPEWA WAKOMA KUMI
(Luka 17:12-14)
Walileta ombi lao kwa Yesu wakitaka kuponywa, Yesu aliwaambia wakajionyeshe kwa makuhani, wakoma walipozingatia ufunuo ule walipona hata kabla ya kufika kwa makuhani.
MFANO WA 3: UFUNUO ALIOPEWA NAAMANI JEMADARI WA JESHI LA SHAMU
(2 Wafalme 5:9-10,14)
Naamani alimjia Nabii Elisha akitaka kuponywa ukoma, Nabii Elisha alipata ufunuo wa kumpa Naamani.
Naamani aliambiwa akaoge kwenye mto Yordani mara saba, alipomaliza mara saba akapona papo hapo.
HITIMISHO
Mungu hujibu maombi kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa njia ya ufunuo, hivyo basi zingatia sana ufunuo Mungu anaokupatia kwa kuwa katika ufunuo huo kuna majibu ya maombi yako.
0 Maoni