✍️Faraja Gasto
Vipo vitu vingi vya kuzingatia katika kufanya huduma, jambo mojawapo ni KUFANYA HUDUMA ENDELEVU.
Huduma endelevu ni nini?
Ni huduma inayogusa kizazi kilichopo na vizazi vitakavyokuja. Yaani kama unaimba sasa nyimbo zako zinapaswa kukihudumia kizazi kingine au vizazi vingine, kama unahubiri mahubiri yako yanapaswa kuhudumia vizazi vitakavyokuja, kama wewe una maono fulani hayo maono yanapaswa kuwa msaada na baraka kwa vizazi vitakavyokuja.
MIFANO YA BIBLIA INAYOTUONYESHA JINSI MUNGU ANAVYOTHAMINI HUDUMA ENDELEVU
MFANO WA 1: KUWARITHISHA WATOTO UFAHAMU KUHUSU MUNGU
(Zaburi 78:5-8)
Mungu aliwaambia waisraeli wafundishe watoto kumjua Mungu, pia watoto wao wawaambie watoto wao yaani kuwepo na mtembeo wa kuhabarishana mambo ya Mungu (matendo yake makuu, matakwa yake, sheria zake nakadhalika).
(Waamuzi 6:11-13)
Wakati Mungu anajifunua kwa Gideoni jambo mojawapo ambalo Gideoni ni "Yako wapi matendo makuu ya Mungu waliyotuhadithia baba zetu?
Hilo swali la Gideoni linatupa kufahamu kuwa wazazi wa kizazi hicho walikuwa na utamaduni wa kuwaambia watoto wao kuhusu Mungu.
MFANO WA 2: KUOKOTA MAWE YA MTO YORDANI
Baada ya wana wa Israeli kuvuka kwenye mto wa Yordani, Mungu aliwaambia kuwa wachukue mawe kumi na mbili ili yawe ukumbusho kizazi baada ya kizazi ili Kila atakayeyaona mawe hayo akiuliza kwa nini yako pale aambiwe kuwa yale mawe yalitokewa kwenye mto Yordani kwa kuwa Mungu aliyakausha yale maji ili wana wa Israeli wapite (Yoshua 4:1-10).
Yale mawe yalikuwa kwa ajili ya kuvipa vizazi habari za matendo makuu ya Mungu.
BAADHI YA MBINU ZA KIBIBLIA ZA KUFANYA HUDUMA ENDELEVU
1.KUANDAA VIONGOZI
Hii ni mbinu ambayo Bwana Yesu aliitumia kufanya huduma endelevu aliandaa mitume kumi na mbili watakaofanya huduma hata kama yeye hayupo.
Hata baada ya Yesu kuondoka tunaona wale mitume waliendeleza kazi ambayo Bwana Yesu aliwaagiza kufanya (Matendo ya mitume 1:2-8)
Musa alihakikisha anakuwa karibu na Yoshua na akamuwekea mikono roho ya hekima ikaingia ndani ya Yoshua (Kumbukumbu la torati 34:9)
Yoshua aliandaliwa kuwa kiongozi ajaye, tunaona huyo Yoshua ndiye Mungu alimtumia kuendelea na kazi aliyoaacha Musa (Yoshua 1:1-5)
2.KUTUNZA KUMBUKUMBU
Kumbukumbu zikitunzwa vizuri zinaweza kuhudumia kizazi kilichopo na vizazi vingine.
Hii ni mbinu Mungu aliitumia ili kuvifanya vizazi vya wana wa Israeli vikumbuke matendo makuu ya Mungu, baada ya wana wa Israeli kuvuka kwenye mto wa Yordani, Mungu aliwaambia kuwa wachukue mawe kumi na mbili ili yawe ukumbusho kizazi baada ya kizazi ili Kila atakayeyaona mawe hayo akiuliza kwa nini yako pale aambiwe kuwa yale mawe yalitokewa kwenye mto Yordani kwa kuwa Mungu aliyakausha yale maji ili wana wa Israeli wapite (Yoshua 4:1-10).
Yale mawe yalikuwa kwa ajili ya kuvipa vizazi habari za matendo makuu ya Mungu.
Baadhi ya mbinu za Kutunza kumbukumbu ni hizi zifuatazo
✓Maandishi (vitabu, makala nakadhalika)
✓Kurekodi sauti na video (kurekodi mahubiri, mafundisho nakadhalika)
✓Kutunza picha za matukio mbalimbali.
HITIMISHO
Ikiwa unataka kufanya huduma endelevu yaani uhudimie kizazi cha sasa na vizazi vijavyo tumia mbinu hizo.
Kama wewe ni muimbaji rekodi nyimbo zako, kama wewe ni muhubiri rekodi mahubiri yako, andika kitabu au vitabu kuhusu ushuhuda wako, namna Mungu alivyokutana na wewe, jinsi Mungu amekutumia kufanya mambo mbalimbali nakadhalika.
0 Maoni