Lengo la somo: ili kuifanya ardhi isiwe kinyume na wewe, iwe upande wako.
UTANGULIZI
Baadhi ya mambo ya msingi ya kufahamu kuhusu ardhi
1. Ardhi ina kinywa (Mwanzo 4:11)(Hesabu 16:30-33)
Kama ardhi ina kinywa basi inaweza kuongea mema au mabaya kutegemeana na sababu mbalimbali.
2. Ardhi ni kiumbe (Mwanzo 1:1)
— Ardhi iliumbwa kwa hiyo ardhi ni kiumbe kama viumbe vingine.
3. Ardhi inaweza kupewa kitu na ikapokea (Mwanzo 4:11)
–Ardhi ilipokea damu ya Habili
—Ardhi inaweza kupokea vitu mbalimbali ili kuwa kinyume na mtu au watu au kuwa upande wa mtu.
4. Ardhi inaweza Kutunza kumbukumbu (Yeremia 22:29-30)
— Ardhi ilitunza kumbukumbu ya maneno aliyotamka Yoshua (Yoshua 6:26) kwamba mtu yeyote atakayejenga mji wa Yeriko atafiwa na watoto wawili, ardhi ilitunza hiyo kumbukumbu aliyejenga Yeriko alifiwa watoto (1 Wafalme 16:34)
5. Ardhi inaweza kumpa mtu kitu au kumnyima (Mwanzo 4:11-12)
—- Kaini aliambiwa akilima ardhi haitampa kitu.
6. Ardhi inaweza kupokea maelekezo kwa ajili ya mtu au watu na ikatekeleza maelekezo hayo.
(Yeremia 22:29-30)
—- Ardhi ilipewa maelekezo ya kuwameza Kora na kundi lake lililoinuka kinyume na Musa na ikatekeleza maelekezo yale (Hesabu 16:30-33)
7. Ardhi inasikia (Yeremia 22:29-30)
— Ardhi iliambiwa andikeni habari za mtu huyu maana yake ni kwamba ardhi inasikia.
NAMNA YA KUBADILISHA LUGHA YA ARDHI ILI ISIONGEE MABAYA KWA AJILI YAKO
1. OMBA REHEMA KWA MUNGU
Yamkini ardhi inaongea mabaya kuhusu wewe kwa sababu ya dhambi au uovu fulani, unapoomba rehema kwa Mungu unainyima ardhi fursa ya kuzungumza mabaya kwa ajili Yako.
(Mwanzo 4:11-12)
Kaini aliua ndugu yake ardhi ikapokea damu Kisha ardhi ikawa kinyume na Kaini.
Ni vema ufahamu kuwa jambo mojawapo ambalo ni kubwa linaloweza kuifanya ardhi kukuongelea vibaya au kuwa kinyume na wewe ni dhambi au uovu.
Rehema za Mungu zikiachiliwa juu Yako, Mungu akikusamehe dhambi au uovu, ardhi inaacha kuongea mabaya kwa ajili yako.
2. IPE ARDHI DAMU YA YESU
Biblia imeweka wazi kuwa ardhi inaweza kupewa na ikapokea, ilipewa damu ya Habili na ikapokea (Mwanzo 4:11) Kisha ardhi ikawa kinyume na Kaini ikawa haiko tayari kumpa kitu (Mwanzo 4:11-12)
Ukiipa ardhi damu ya Yesu Kristo, ni damu inayonena mema (Waebrania 12:24) ardhi lazima ikuzungumzie mema kwa kuwa imepokea damu inenanyo mema.
3. IAMBIE ARDHI IONGEE NINI KWA AJILI YAKO
(Yeremia 22:30)
Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Ardhi iliambiwa iandike hayo mambo kwa ajili ya mtu huyo.
Hivyo basi ardhi inaweza kuambiwa nini cha kufanya na ikafanya kwa kuwa tuliookoka tuna haki ya kisheria katika ulimwengu wa roho kumiliki ardhi (Ufunuo 5:10) mmiliki anaweza kuamua nini aiambie ardhi.
Barikiwa kwa haya machache.
0 Maoni