(Isaya 41:15)
UTANGULIZI
Msisitizo: Mungu anataka vifaa vikali kwa ajili ya kazi zake mbalimbali hapa duniani, Mungu hataki vifaa butu.
Sifa za kifaa kikali
1.Kimenolewa.
2.Kinachoma.
3.Kina makali.
4.Kinakata kwa urahisi.
5.Hautumii nguvu nyingi ukiwa na kifaa kikali.
Kwa nini Mungu atake vifaa vikali?
1.Kifaa kikali kinakata kwa urahisi.
2.Kifaa kikali kinapenya kwa urahisi.
3.Kifaa kikali hakichezewi bali kinaogopwa ili kisidhuru.
— Mungu hataki tuchezewe na shetani anataka tuwe tishio, tuwe kichomi kwa shetani.
—-Mara nyingi shetani amewachezea watu kwa kuwa sio wakali, ni vifaa butu havina madhara Kwa shetani.
Kwa mfano moto unaweza kuwa mkali au wa kawaida, panga linaweza kuwa kali au butu, jembe linaweza kuwa kali au butu, shoka linaweza kuwa kali au butu.
Vivyo hivyo watumishi wanaweza wakawa wakali au butu, vivyo hivyo vyombo vya Mungu vinaweza vikawa vikali au butu.
Ndio maana nafundisha somo hili ili uwe mtumishi wa Mungu au kifaa cha Mungu kikali kwa kuwa Mungu anataka vifaa vikali.
MAMBO YATAKAYOKUSAIDIA UWE KIFAA KIKALI
1.WEKA NENO LA MUNGU MOYONI MWAKO KWA WINGI
(Waebrania 4:12)
Sifa mojawapo ya neno la Mungu ni kwamba "neno la Mungu lina ukali kuliko upanga woote ukatao kuwili" neno la Mungu kwa kuwa ni Kali linaweza kuchoma (Matendo ya mitume 2:37)
Ukiwa na neno la Mungu ndani yako linakufanya kuwa chombo kikali kwa kuwa neno ni kali sana kuliko upanga wowote ukatao kuwili.
2.TAKA SANA KUJAA ROHO MTAKATIFU KILA WAKATI
Roho wa Mungu anaweza kukufanya usiwe butu, anaweza kukufanya uwe kifaa kikali kabisa.
Kadiri unavyozidi kujaa Roho Mtakatifu ndivyo unavyozidi kuwa tishio kwa shetani.
Wanafunzi wa Yesu walipojaa Roho Mtakatifu tunaona Mtume Petro alihubiri injili watu wakachomwa mioyo yao (Matendo ya mitume 2:37)
Mtu aliyejaa Roho Mtakatifu ni tishio kwa shetani, ni chombo kikali sana.
3.UWE MTU WA MAOMBI
— Maombi huwa yananoa, wale waliokuwa butu (waoga, wenye mashaka n.k) wakiingia kwenye maombi wanatoka wakiwa wakali kwa kuwa wamenolewa.
(Matendo ya mitume 4:23-31)
Mitume walipotishiwa waliogopa wakapiteza kabisa ujasiri wa kuhubiri injili, ilibidi waitishe maombi, kanisa likaanza kumwomba Mungu.
Walipomuomba Mungu Biblia inasema "wakajaa Roho Mtakatifu Kisha wakapata ujasiri wa kuhubiri"
NB: Kifaa butu, hakina jitihada za maombi, hakina kiu ya kujaa Roho Mtakatifu pia hakuna neno la Mungu.
Barikiwa kwa haya machache, Mungu akusaidie usiwe kifaa butu, uwe mkali.
0 Maoni