IMANI KAMA KIFAA CHA UOKOZI



✍️Faraja Gasto

UTANGULIZI

Ukisoma katika Biblia imani inaitwa NGAO (Waefeso 6:16)

Kazi ya ngao ni kumkinga mtu dhidi ya mashambulizi fulani nakadhalika.

Hivyo basi kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa kama imani ni ngao basi imani ni kifaa cha kiroho chenye kazi mbalimbali ikiwemo kumuokoa mtu.

MIFANO YA BIBLIA KUHUSU IMANI KAMA KIFAA CHA UOKOZI

MFANO WA 1: IMANI ILIVYOMUOKOA RAHABU YULE KAHABA WA YERIKO

(Waebrania 11:31)

Biblia inasema "kwa imani Rahabu hakuangamia" 

Biblia inataka tufahamu kuwa kilichomuokoa Rahabu asiangamizwe ni imani kwa hiyo Imani inaweza kumuokoa mtu.

MFANO WA 2: IMANI ILIVYOMUOKOA MWANAMKE MWENYE DHAMBI

(Luka 7:50)

Mwanamke fulani mwenye dhambi alimwendea Yesu akasamehewa dhambi zake, Yesu akamwambia "imani yako imekuokoa" 

Unaweza kujiuliza imani ilimuokoa na nini? 

Imani ilimuokoa na hukumu ya dhambi kwa kuwa tunafahamu kwa mujibu wa Biblia kuwa hukumu ya Mungu ipo kwa ajili ya wenye dhambi, mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23)(Yakobo 1:15)

Kwa hiyo kwa tafsiri nyingine ni sawa na kusema imani ilimuokoa na mauti ambayo ni mshahara wa dhambi.

MFANO WA 3: IMANI ILIVYOWAOKOA SHADRAKA, MESHAKI NA ABEDNEGO

(Danieli 3:16,17, 23-26)

Hao Vijana watatu walikuwa na imani, walijua kwa imani Mungu anaweza kuwaokoa na chochote ikiwemo moto.

Walipotupwa kwenye tanuru la moto hawakuteketea kwa sababu imani iliwaokoa.

Barikiwa kwa haya machache.




Chapisha Maoni

0 Maoni