MOYO MGUMU: CHANZO CHA KUKWAMA KWA MAMBO MBALIMBALI - Seh ya 2


✍️Faraja Gasto

Katika sehemu ya kwanza nilikufundisha na tulifahamu namna moyo mgumu unavyokwamisha mambo mbalimbali, katika sehemu hii ya pili ambayo ni mwisho Nataka nikufundishe mbinu baadhi za kushughulikia ugumu wa moyo.

MBINU YA 1: WEKA NENO LA MUNGU MOYONI MWAKO PIA WEKA NENO LA MUNGU KWENYE MIOYO YA WATU KWA NJIA YA KUFUNDISHA

(Zaburi 119:11)

Biblia inatupa kufahamu kuwa neno linaweza likawekwa moyoni na likatenda kazi, Daudi alisema aliweka neno moyoni ili asitende dhambi, watu wengi wanaposikia neno dhambi katika nafsi zao kunakuja picha mbalimbali kwa mfano kuzini, kuua, kuiba nakadhalika.

Lakini ni vema ufahamu kuwa ugumu wa moyo ni chanzo kimojawapo cha dhambi nyingi sana, kwa hiyo Daudi aliposema nimeliweka neno ili nisikutende dhambi maana mojawapo ni kwamba Daudi aliweka neno moyoni liondoe ugumu wa moyo unaopelekea watu kutenda dhambi ndio maana alisema "ILI NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI"

(Yeremia 23:29)

Neno la Mungu limefananishwa na moto na nyundo ivunjayo mawe vipande vipande maana yake ni kwamba neno la Mungu linaweza kuvunja vitu vigumu ikiwemo ugumu wa mioyo, Mungu aliwaambia wana wa Israeli nitawaondolea moyo wa jiwe (Ezekieli 35:26), mbinu mojawapo ambayo Mungu anaitumia kushughulikia vitu vigumu ni neno, Mungu hutumia neno lake kushughulikia vitu vigumu ikiwemo ugumu wa moyo.

NB: Ili tuweze kushughulikia ugumu wa mioyo ni vema tuweke neno la Mungu mioyoni mwetu na tuwafundishe watu neno la Mungu maana neno lina uwezo wa kuondoa ugumu wa mioyo.

MBINU YA 2: KUMUOMBA MUNGU KUHUSU MIOYO YETU NA YA WATU WENGINE

Kama Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu (Kutoka 7:3) basi Mungu anaweza kuuondoa ugumu wa moyo ndani ya mtu.

Ifahamike kuwa hata shetani anaweza akaufanya moyo wa mtu kuwa mgumu , Kwa hiyo tunaweza kumuomba Mungu amuondolee mtu fulani ugumu wa moyo na Mungu akajibu hayo maombi.

Pia unaweza kujiombea mwenyewe ikiwa kuna ugumu wa moyo ndani yako Mungu auondoe ili usije ukakwamisha mambo mbalimbali.

Jambo mojawapo ambalo Daudi alifanya ni kuomba Mungu amuumbie moyo safi (Zaburi 51:10), hata wewe unaweza kumuomba Mungu kuhusu moyo wako.

Barikiwa na BWANA YESU. 



 

Chapisha Maoni

0 Maoni