TIMIZA WAJIBU WAKO KATIKA KIZAZI CHAKO


                      ✍️ Faraja Gasto

Matendo ya Mitume 13:36

[36]Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. For David, after he had served his own generation by the will of God, fell on sleep, and was laid unto his fathers, and saw corruption.

Mungu ametuumba ili tufaidiane yaani uwepo wako uwe na faida kwa wengine na uwepo wa wengine uwe na faida kwako ndio maana chochote ambacho Mungu anakupa, anakupa Kwa faida ya ufalme wake, kwa faida yako na faida ya wengine.

Mungu amekuweka kwenye kizazi hiki ili utimize wajibu fulani katika kizazi hiki haijalishi unajua wajibu huo au haujui wajibu huo, wengine wamewekwa kwenye kizazi hiki wawe viongozi wa kiroho na kiserikali, wengine wamewekwa wawe wafungua milango ili watu wengine wapite kwenda mahali fulani Mungu anapotaka wafike, wengine wamewekwa wawe watengeneza njia ili wengine wapite waende mahali Mungu anataka, wengine wamewekwa kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye kizazi husika, wengine wamewekwa kwenye kizazi ili kulea kizazi (si kila mzazi ni mlezi, kuzaa ni kitu kingine na kulea na kitu kingine), hayo ni baadhi ya makusudi ya Mungu Kwa watu mbalimbali.

Je! unajua wajibu wako katika kizazi chako?

MAANA YA KULITUMIKIA SHAURI LA MUNGU

Kulitumikia shauri la Mungu ni KUTIMIZA WAJIBU WAKO KATIKA KIZAZI CHAKO AU NI KUTIMIZA WAJIBU AMBAO MUNGU AMEKUPA KWA AJILI YA KIZAZI CHAKO.

Matendo ya Mitume 13:36

Biblia inasema Daudi akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake akafa, yaani Daudi alikufa baada ya kutimiza wajibu wake katika kizazi chake.

MAMBO MAKUU YA KUFANYA ILI UTIMIZE WAJIBU WAKO KATIKA KIZAZI CHAKO

1. OKOKA (MWAMINI YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI)

Unajua kwa nini ni muhimu sana kuokoka ni kwa sababu "TULIUMBWA KATIKA KRISTO YESU ILI TUTENDE MEMA" (Waefeso 2:10)(Wakolosai 1:16). Maana mojawapo ya kutenda mema ni kutimiza wajibu wako katika kizazi chako, yaani wajibu ambao Mungu anataka uutimize utautimiza endapo utakuwa ndani ya Yesu Kristo tu si vinginevyo.

Unapoingia ndani ya Yesu Kristo unaanza kuwa halisi na kuna namna Mungu ataanza kukufunua jinsi unavyotakiwa kuwa Katika dunia hii, yaani wewe unakuwa halisi unapokuwa ndani ya Yesu Kristo.

2. OMBA MUNGU AKUJULISHE WAJIBU WAKO KATIKA KIZAZI HIKI

Matendo ya Mitume 13:36 

Kama Daudi alitimize wajibu wake Katika kizazi chake maana yake ni kwamba Mungu alimwambia anachopaswa kufanya Katika kizazi chake.

NB

1. Mungu hakukuumba ili usome sana na kupata Kazi MUNGU ALIKUUMBA UTIMIZE WAJIBU WAKO KATIKA KIZAZI CHAKO. Simaanishi si mapenzi ya Mungu usome sana.

2. Mungu hakukuumba ili uolewe au uoe tu bali MUNGU ALIKUUMBA UTIMIZE WAJIBU WAKO KATIKA KIZAZI CHAKO. Simaanishi si mapenzi ya Mungu uoe au uolewe.

3. Mungu hakukuumba ili ufanikiwe kuwa na fedha nyingi na mali bali MUNGU ALIKUUMBA UTIMIZE WAJIBU WAKO KATIKA KIZAZI CHAKO. Simaanishi si mapenzi ya Mungu ufanikiwe.

4. Hata kama umeokoka fahamu kuwa kuna wajibu wako unaopaswa kutimiza Katika mwili wa Kristo (kanisa) Kuna wajibu unaopaswa kutimiza Katika kizazi chako.


Chapisha Maoni

0 Maoni