MAOMBI KAMA UTUMISHI

                        ✍️Faraja Gasto

Katika ufalme wa Mungu kuna utumishi wa aina mbalimbali, aina mojawapo ya utumishi ni UTUMISHI WA MAOMBI au Kwa lugha rahisi ni MAOMBEZI. Utumishi huu unahusu kuwaombea watu Kwa Mungu, kuombea vitu, kuombea maeneo nakadhalika.

Utumishi huu ni utumishi huu unapaswa kufanywa na kila raia wa ufalme wa Mungu Kwa kuwa huu ni utumishi kama aina zingine za utumishi Katika ufalme wa Mungu.

BAADHI YA WATU WALIOFANYA UTUMISHI WA MAOMBI

1. NABII ANA FANUELI 

Luka 2:36-37)

Mojawapo ya utumishi alioufanya Nabii Ana Fanueli ni utumishi wa maombi au utumishi wa kuombea ajenda mbalimbali mbele za Mungu.

2. EPAFRA

(Wakolosai 4:12-13)

Mtumishi wa Mungu Epafra alikuwa akifanya bidii kuwaombea wakristo waliokuwa Katika kanisa la Kolosai, Hierapoli na Laodikia, Epafra alitaka kuona wakristo wakiwa wakamilifu na kuthibitika sana Katika mapenzi yote ya Mungu.

3. BWANA YESU

(Luka 22:31-32)(Yohana 17:9,17-17)

Bwana Yesu alikuwa akiombea watu pia alikuwa akiombea mambo mbalimbali pindi alipokuwa hapa duniani, mpaka sasa bado Bwana Yesu anatuombea kwa Baba yetu wa mbinguni.

4. MUSA

(Zaburi 106:23)

Musa alikuwa akiwaombea sana wana wa Israeli ili Mungu asiwaangamize kutokana na uasi wao.

5. MTUME PAULO 

(Waefeso 1:15-23)

Mtume Paulo alikuwa akiombea watu mbalimbali, miongoni mwa watu walioombewa na Mtume Paulo ni wakristo wa kanisa la Kule Efeso, jambo mojawapo alilowaombea ni kwamba Mungu awape roho ya hekima na ufunuo katika kumjua Mungu pia macho ya mioyo yao yatiwe Nuru.

NB: Utumishi huu wa maombi ni wa muhimu sana kama ulivyo utumishi wa aina zingine, ni vema kila raia wa ufalme wa Mungu kuufanya Utumishi huu kwa kuwa kuna watu Mungu atawaponya endapo utaomba, Kuna watu wataokolewa endapo utaomba, Kuna watu watainuliwa kihuduma, kiuchumi nakadhalika endapo utaomba, Kuna watu watasimama imara kiroho endapo utaomba, Mungu atafunua mambo mbalimbali endapo utaomba, Mungu atawavusha watu kutoka walipokwama endapo utaomba, nchi itaponywa endapo utaomba, misingi ya vizazi vingi itainuka endapo utaomba, watumishi watafanya mambo makubwa endapo utawaombea. MAOMBI YAKO NI YA MUHIMU SANA HIVYO BASI USIPUUZE UTUMISHI HUU.

Chapisha Maoni

0 Maoni