TAFUTA NAFASI


                     ✍️ Faraja Gasto

(Luka 22:6)

Kuna mambo mengi ya kujifunza katika kisa cha Yuda Iskariote kumsaliti Bwana Yesu, jambo mojawapo ninalotaka kufundisha ni KUTAFUTA NAFASI AU KUTAFUTA FURSA (seeking an opportunity).

Neno nafasi Kwa lugha nyingine ni fursa Kwa hiyo kama Yuda Iskariote alitafuta nafasi ya kumsaliti Bwana Yesu maana yake ni sawa na kusema kwamba YUDA ALITAFUTA FURSA YA KUMSALITI BWANA YESU.

Ukisoma kitabu cha Luka sura ya ishirini na mbili mstari wa Sita utaona shetani alipomwingia Yuda Iskariote, Yuda ALIANZA KUTAFUTA NAFASI AU FURSA YA KUMSALITI YESU.

IKO HIVI: Si kila fursa utaipata Kwa urahisi Kuna fursa zingine unapaswa kuzitafuta ndio maana nakuambia TAFUTA NAFASI AU FURSA, ukisubiri fursa zije zenyewe utachelewa sana kuzipata ANZA KUZITAFUTA.

NI MUHIMU UZINGATIE HAYA

Kama Yuda alitafuta fursa ya kumsaliti Bwana Yesu ni Sawa na kusema kwamba watu wasiomwamini Bwana Yesu wanafanya juhudi nyingi za kutafuta fursa kuhakikisha watu hawamwamini Yesu, watu hawaendi kanisani, watu hawasomi Biblia, watu hawaombi, makanisa yanavunjika nakadhalika.

KWA HIYO WEWE KAMA MWAMINI AU MTU ULIYEMWAMINI YESU

1. Tafuta fursa za kujenga ufalme wa Mungu, tafuta wapi kanisa la Mungu linajengwa wekeza nguvu zako hapo, wekeza fedha hapo,  tafuta watumishi wanaotumika katika mazingira magumu washike mkono kwa kuunga mkono kazi wanazofanya (support) n.k

2. Tafuta fursa za kupeleka injili, tafuta wapi panahitaji injili peleka injili hapo,  wekeza fedha injili ihubiriwe hapo, wanunulie watumishi vyombo wakahubiri injili hapo.

3. Tafuta fursa za kutenda mema, tafuta wajane, yatima na watu wanaoishi katika mazingira magumu waonyeshe ukarimu kwa kuwapatia mahitaji yao nakadhalika.

NB: Yuda Iskariote ALITAFUTA FURSA YA KUMSALITI YESU, WEWE ULIYEMWAMINI YESU TAFUTA FURSA ZA KUUJENGA UFALME WA MUNGU, TAFUTA FURSA ZITAKAZOSABABISHA JINA LA YESU LI 'MAKE HEADLINE, TAFUTA FURSA ZA KUTENDA MEMA NAKADHALIKA.

Chapisha Maoni

0 Maoni