✍️ Faraja Gasto
(Mathayo 21:45-46)
Yesu alipokuwa akifundisha neno la Mungu liliwagusa mafarisayo na wakuu wa makuhani lakini BADALA YA KUTUBU WAKATAFUTA KUMKAMATA.
(Luka 11:45)
Neno la Mungu lilipowagusa wanasheria badala ya kutubu walimchukulia Yesu kama mpinzani wao.
Ndivyo ilivyo hata sasa watu wengine wanapoguswa na neno la Mungu hawachukui hatua kama neno lilivyowagusa, wengine huanza kusema mtumishi anafuatilia maisha yangu, mtumishi anapenda kuhubiri maisha ya watu badala ya kuhubiri neno, nitahama hili kanisa Kwa kuwa watumishi wanapenda kuzungumzia maisha yangu.
NB: Kama uko kwenye kundi hilo fahamu kuwa uko kwenye hatari (hauko Salama) Kwa kuwa neno la Mungu linapokugusa unapuuza mguso huo na kuanza kuwatuhumu watumishi, kuwadharau au kuwachukia watumishi.
NENO LA MUNGU LINAPOKUGUSA FANYA HIVI
Chukua hatua Kutegemeana na ulivyoguswa na hilo neno la Mungu.
° Kama neno la Mungu limekugusa linalohusu toba basi TUBU.
° Kama neno la Mungu limekugusa linalohusu utoaji wa sadaka Fulani ANZA KUTOA SADAKA HIYO AU SADAKA HIZO.
° Kama neno la Mungu limekugusa linalohusu msamaha basi SAMEHE.
° Kama neno la Mungu limekugusa linalohusu kuhubiri injili ANZA KUHUBIRI INJILI, ANZA KUTOA FEDHA NA VIFAA ILI INJILI IENDE KWA WALENGWA.
Soma mifano hii michache
(Matendo ya mitume 2:37-41)
Hawa watu walipoguswa na neno la Mungu waliuliza tufanyeje? Walipoambiwa watubu WALITUBU.
(Ezra 10:9-19)
Wana wa Israeli walipoguswa na neno la Mungu walichukua hatua kama neno la Mungu lilivyowaelekeza.
0 Maoni