IFAHAMU SIRI HII YA KUTOKUELEWEKA


                       ✍️ Faraja Gasto

Umeshawahi kujiuliza maswali haya

1. Mtoto mchanga wa wiki moja anapokuwa tumboni anafafana vipi?

2. Inachukua muda gani mtoto aliye tumboni kuanza kuvutia?

3. Kabla mtu hajapuliziwa pumzi ya Mungu alikuwa anafananaje?

NINACHOTAKA KUKUFUNDISHA NI HIKI

Katika maisha Kuna wakati wa kutoeleweka, yaani watu wakikutazama hawakuelewi, watu wakikusikia hawakuelewi hata ukijitahidi kuwafafanulia mipango, maono na malengo hawakuelewi kabisa Kwa sababu KUTOKUELEWEKA ni sehemu ya maisha hata mimba inapotungwa ndani ya tumbo, ukipata nafasi ya kuangalia ndani ya tumbo huwezi kuvutiwa na huyo mtoto huwezi kuelewa kwa haraka ni wa kike au wa kiume mpaka baada ya muda fulani ndio anaanza kueleweka na kuvutia.

Kwa hiyo chochote unachokipanga au kukikusudia, maono uliyonayo na malengo uliyonayo ni kama ujauzito wa wiki moja usishangae kuona watu hawayaelewi maono yako, mipango na malengo uliyonayo, KUTOKUELEWEKA NI SEHEMU YA HATUA ZA MAISHA.

Umeshawahi kutafakari Mwanzo 2:7

Mungu alimuumba mtu kwa mavumbi ya ardhi kisha akampulizia pumzi yake ndipo mtu akaanza kuvutia, jaribu kufikiri kabla mtu hajapuliziwa pumzi ya uhai alikuwa anafanana vipi? naamini alikuwa hana mvuto pia alikuwa haeleweki.

Nami nakumbia usiyatupilie mbali maono, mipango na malengo yako kwa kuwa watu hawakuelewi, tembea Katika maono hayo WATAKUELEWA BAADAYE ukitaka kila mtu ayaelewe maono yako au mipango yako ndio uanze kutembea kwenye maono hayo HAUTAWAHI KUTEMBEA KWENYE MAONO HAYO Kwa kuwa utavunjwa moyo, utadhihakiwa pia utaonekana umepata Shida kwenye akili.

NB: Maadamu Mungu ameyaelewa hayo maono au hiyo mipango, maadamu wewe umeyaelewa maono yako tembea kwenye maono hayo WATU WATAKUELEWA BAADAYE.


Chapisha Maoni

0 Maoni