✍️Faraja Gasto
Kuna aina kuu tatu za watumishi
1. Walioitwa na Mungu (waliowekwa na Mungu)
°°°Hawa wana mwelekeo wa huduma au utumishi wao (focus) Kwa kuwa wanajua walichoitiwa kukifanya.
2. Waliojiita (waliojiweka kwenye utumishi)
°°°Hawa waliingia kwenye utumishi ili kupata vitu (material things), hawa ndio wale ambao Biblia inasema "mungu wao ni tumbo" (Wafilipi 3:18), wengine waliingia utumishi kwa kuwa Mungu aliwatumia kufanya jambo Fulani wakadhani wameitwa kumbe Mungu aliwatumia tu.
3. Walioitwa na wanadamu au waliowekwa na wanadamu
°°°Kundi hili linahusisha wale ambao wanapelekwa na taasisi (dhehebu) wakaanzishe makanisa au huduma sehemu fulani kwa kuwa taasisi imeona vema kuanzisha huduma mahali fulani nakadhalika.
NB:
1.Mungu akikuita lazima atakuambia alichokuitia, ukifanya ambacho hakukuambia kufanya utakuwa unajitumikia mwenyewe sio Mungu. Soma mifano hii ya baadhi ya watu walioitwa na Mungu
°Musa (Kutoka 3:10)
° Yeremia (Yeremia 1:5-7)
° Petro na Andrea (Mathayo 4:19)
2. Taasisi inapokupeleka kufanya huduma mahali fulani ukitekeleza maelekezo ya taasisi utakuwa unaitumikia taasisi sio Mungu.
3. Kumtumikia Mungu ni zaidi ya kuwa Mtume, Nabii, Mwalimu, Mwinjilisti, Mchungaji, Muimbaji nakadhalika, KUMTUMIKIA MUNGU NI KUFANYA YANAYOMPENDEZA MUNGU, NI KUFANYA ALIYOAGIZA AU ALIYOELEKEZA MUNGU. Unaweza ukawa Mtume lakini ukawa hautumikii Mungu, unaweza ukawa mchungaji lakini ukawa hautumikii Mungu, unaweza ukawa Mwalimu lakini ukawa hautumikii Mungu,unaweza ukawa Nabii lakini ukawa hautumikii Mungu,unaweza ukawa Mwinjilisti lakini ukawa hautumikii Mungu, ndio maana Yesu alisema "wengi wataniambia siku ile Bwana tulifaanya unabii kwa jina lako, Bwana tulifanya miujuza mikubwa kwa Jina lako.................halafu Yesu atajibu SIKUWAJUA KAMWE , ONDOKENI KWANGU MTENDAO MAOVU (Mathayo 7:22-23).
Anaposema hakuwajua haimaanishi kuwa hajui majina yao bali HAWATAMBUI KUWA NI WATUMISHI WAKE, Kwa maana nyingine ni Sawa na kusema WATUMISHI WANGU NAWAJUA NYIE NI AKINA NANI?
4. Mungu anapomuita mtu huwa anamuita kwa jina lake na anatambua majina ya wote aliowaita
Soma mifano hii
°°°° Musa (Kutoka 3:4)
°°°° Samweli (1 Samweli 3:10)
5. Kutumiwa na Mungu haimaanishi Mungu amekuita, Mungu anaweza kukutumia hata kama hajakuita kwenye utumishi.
6. Si kila anayekwenda au anayepelekwa chuoni (Bible colleges, Schools of ministry e.t.c) ameitwa na Mungu, kwa hiyo wito haupimwi kwa vyeti vya chuoni.
Baada ya kuyafahamu hayo jiulize uko kwenye kundi gani?
0 Maoni