1. Kuchekwa.
Ukianza hatua za awali za kuyafikia mafanikio si ajabu ukasikia sauti zikikucheka Tena si ajabu ukachekwa hata na watu ambao ukiwatazama utawahurumia lakini si ajabu wakakucheka.
2. Kudharauliwa.
Usipodharau kudharauliwa huwezi kufanikiwa Kwa hiyo kudharauliwa ni sehemu ya maisha, ukianza hatua za awali za kuelekea kwenye mafanikio utakumbana na jambo linaitwa kudharauliwa.
3. Kupuuzwa.
Ukianza hatua za awali za kuelekea kwenye mafanikio usishangae watu wakakupuuza, ukiwaambia jambo watakupuuza.
4. Kukonda.
Yapo mambo mengi yanayowafanya watu kukonda, jambo mojawapo linalowafanya watu kukonda ni hatua za awali za kuyafikia mafanikio.
5. Kutoeleweka.
Ukianza safari kuelekea kwenye mafanikio watu hawatakuelewa, iko hivi mimba inapotungwa ndani ya tumbo ukitazama huko ndani ya tumbo mtoto huwa haeleweki huwa anaanza kueleweka baada ya miezi kadhaa ndivyo ilivyo katika maisha kuna wakati watu hawawezi kukuelewa lakini Kadiri unavyosonga mbele watu wataanza kukuelewa.
6. Kuvunjwa moyo.
Niulize mtu yeyote aliyefanikiwa atakuambia Kuna wakati alivunjwa moyo, alikatishwa tamaa kwa njia mbalimbali.
7. Kutishwa.
Utatishiwa kuwa ukifunga na kuomba madonda ya tumbo yatakusumbua, ukifanya hiyo biashara utapata hasara, ukisoma hiyo kozi hautapata kazi nakadhalika.
NB: Ukiona hayo yanatokea fahamu kuwa uko kwenye barabara ya kuelekea kwenye mafanikio kwa hiyo unapigwa vita usifikie kwenye mafanikio, kitakachokusaidia ni KUKAZANA NA KUSONGA MBELE, LAKINI HAKIKISHA UNACHOKIFANYA NI CHA HALALI NA HAKI.
0 Maoni