Mungu alituumba kwa namna ambayo kila mtu anahitaji mtu au watu ili aweze kufanikiwa katika mambo mbalimbali, Kwa hiyo haijalishi una elimu ya kiwango gani, una uwezo wa kiuchumi kiasi gani, una upako kiasi gani fahamu kuwa unahitaji mtu au watu wa aina mbalimbali katika mazingira mbalimbali.
Soma mifano hii michache
(Mwanzo 2:18,21-23)
Mungu aliona Adamu anahangaika kwa majukumu mengi kwa hiyo Mungu akaamua kumfanyia Adamu msaidizi au mtu wa kumsaidia.
(Mathayo 18:19)(Danieli 2:17-19)
Kuna maombi ambayo yanahitaji watu kuanzia wawili nakuendelea kwa hiyo usije ukadhani hauhitaji watu wa kuomba nao, jifunze kuwa na timu yako binafsi ya maombi yaani uwe na watu unayoweza kuwashirikisha jambo mkaliombea.
NB: Mtu anayetaka kufanya mambo peke yake HAJAWAHI KUFANIKIWA, UNAHITAJI MTU AU WATU.
0 Maoni