(Mithali 6:6-8)
NB: Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya hekima ya Mungu na uwezo wa kufikiri.
Biblia inampa ushauri mtu mvivu Kwa kumwambia hivi "ewe mvivu mwendee chungu ZITAFAKARI NJIA ZAKE UKAPATE HEKIMA"
Biblia inataka tufahamu kuwa mvivu ana uwezo mdogo wa kufikiri, uvivu unapunguza uwezo wa kufikiri, uwezo mdogo wa kufikiri ni matokeo ya uvivu pia uvivu ni matokeo ya kukosa hekima. Kwa hiyo ili mtu aongeze uwezo wake wa kufikiri anatakiwa apate hekima ndio maana kazi mojawapo ya hekima ya Mungu ni kuongeza uwezo wa kufikiri.
(1 Wafalme 3:128)
Mara baada ya Mfalme Sulemani kupewa hekima na Mungu, Mfalme Sulemani alijikuta amepata uwezo mkubwa wa kufikiri, siku moja akaletewa kesi ili aamue, kiuhalisia ukisoma kesi Ile ilikuwa kesi ngumu sana kuiamua lakini kutokana na hekima ya Mungu iliyokuwa ndani ALIYAPIMA maneno ya mshitaki na mshitakiwa na akapambanua yupi ni mwenye haki yupi hana haki. Kama Mfalme Sulemani angekuwa na uwezo mdogo wa kufikiri asingeweza kuiamua Ile kesi.
NB: Kwa mujibu wa Biblia chanzo kimojawapo cha kuchelewa Kwa hukumu za kesi ni mahakimu au Majaji kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na hiyo inasababishwa na kukosa hekima ya Mungu Kwa hiyo kumbuka kuwaombea hekima.
Barikiwa.
0 Maoni