UMUHIMU WA KUWEKEZA KWA VIJANA KWA MASLAHI YA TAIFA


                        Faraja Gasto


Vijana wamepewa majina mengi ikiwemo NGUVU KAZI YA TAIFA.


Ukweli ni kwamba NGUVU KAZI ISIYO NA KAZI HAINA MANUFAA KWA TAIFA bali inazalisha matatizo katika nchi.


Mtu mwenye hekima aliwahi kusema "fahari ya vijana ni nguvu zao" (Mithali 19:29a), vijana wakitumia nguvu zao vibaya ni hatari kwa taifa.


Kila taifa linapaswa kuandaa mipango ya kuzitumia nguvu za vijana kwa maslahi ya taifa, hili linatakiwa kwenda sambamba na

1. Kuhakikisha vijana wana kazi rasmi na zisizo rasmi maadamu ni kazi halali.


2. Kuwafungulia vijana njia na milango ili wapate fursa za ajira, elimu nakadhalika.


3. Kuwapa vijana nyenzo za ajira, elimu na nyenzo zitakazowawezesha kushiriki katika ujenzi wa taifa. Nyenzo kama vile elimu, vifaa, fedha nakadhalika.


UMUHIMU

1. Taifa litatengeza viongozi na vijana wazalendo.


2. Mzunguko wa fedha utaongezeka katika nchi.


3. Ulinzi na usalama utadumishwa katika nchi.


4. Maendeleo ya jamii.

Chapisha Maoni

0 Maoni