Ukisoma Biblia utagundua sadaka ina nguvu za ajabu, sadaka inaweza kulinda, sadaka inaweza kufunga au kufungua mtu au mambo mbalimbali, sadaka inaweza kufunua au kufunika mambo au mtu, sadaka inaweza kutumika kama silaha n.k ndio maana ni muhimu sana kutoa sadaka kwa Mungu, sadaka za aina mbalimbali.
Nataka nikufundishe kuhusu sadaka kama silaha, nianze kwa kukupa tafsiri kuhusu neno "silaha" kwa mujibu wa kamusi mbalimbali.
Ukisoma kamusi mbalimbali utaona kuwa silaha ni kitu au chombo chochote kinachoweza kulinda, kudhuru n.k
(1 Samweli 7:7-11)
Kabla waisraeli hawajapigana na wafilisti, Samweli alitoa sadaka, sadaka iliwatengenezea ushindi waisraeli.
(1 Wafalme 18:30-40)
Nabii Eliya alipokuwa akikabiliana na timu Baali, Eliya alitoa sadaka, sadaka ilimtengenezea ushindi Nabii Eliya.
(Hesabu 22:39, 23:1-3)
Mfalme wa Moabu alipotaka kukabiliana na waisraeli, Mfalme wa Moabu alitoa sadaka.
NB: Jizoeze na jifunze kutoa sadaka kabla haujamuomba Mungu, sadaka ina nguvu za ajabu.
0 Maoni