Ukisoma Biblia utagundua kuwa imani ni lango mojawapo linalopitisha mambo mengi kama vile nguvu za Mungu, miujiza, uponyaji, hekima nakadhalika (Mathayo 8:22, Mathayo 8:29-30)(Yakobo 1:5-7)
Nataka nifundishe kidogo "imani kama lango la maarifa"
(Waebrania 11:23)
Imani ndio ilimsaidia mama Musa kupata maarifa ya kumficha Musa kwa muda wa miezi mitatu, imani ilimsaidia mama Musa kutengeneza kisafina chenye uwezo wa kuelea juu ya maji ili kumuhifadhi Musa (Kutoka 2:2-3)
NB: Ni rahisi kuficha mimba ya miezi mitatu ila sio rahisi kumficha mtoto mchanga kwa miezi mitatu ndio maana Biblia inatuambia alipata maarifa kwa imani.
(Waebrania 11:31)
Imani ilimsaidia Rahabu kahaba wa Yeriko kupata maarifa ya kuwaficha wapelelezi na kufanya nao agano lililopelekea akawa salama yeye na familia yake na mali zao (Yoshua 2:4-21)
NB: Imani itakusaidia kupata maarifa ya kukusaidia hata katika nyakati ngumu ili ujikwamue ulipokwama, ili usiangamie wakati wengine wanaangamia nakadhalika.
0 Maoni