Tunaposikiliza habari za Mungu huwa ndani yetu kunaingia imani (Warumi 10:17)
Kila imani inayoingia mioyoni mwetu huwa inakuja na WAZO AU MAWAZO ambayo Mungu hutaka tuyatendee kazi japo sio wote huyatendea kazi mawazo hayo.
(Marko 5:25-34)
Mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa na damu miaka 12 aliposikia habari za Yesu ndani yake kuliingia imani, IMANI ILIKUJA NA WAZO LA KUGUSA VAZI LA YESU.
Alipotendea kazi lile wazo aliponywa ugonjwa aliokuwa nao.
(Kutoka 18:8-27)
Yethro aliposimuliwa habari za matendo makuu ya Mungu ndani yake kuliingia imani (akamwamini Mungu wa waisraeli)
ILE IMANI ILIKUJA NA WAZO LA KUMTOLEA MUNGU SADAKA NA DHABIHU, ile sadaka na dhabihu aliyotoa ilifungua mlango wa kupewa neno la hekima kwa ajili ya utumishi wa Musa.
Lile neno la hekima likampunguzia Musa mzigo wa kuwahudumia wana wa Israeli.
HITIMISHO
Wazo unalolipata wakati unasikiliza neno au habari za Mungu litendee kazi.
0 Maoni