KUSHUGHULIKIA TABIA ZA WATOTO KWA MBINU ZA KIBIBLIA


                        Faraja Gasto


Lengo la somo: ili uwe na watoto watakaokustarehesha na kukufurahisha nafsi yako (Mithali 29:17)


UTANGULIZI

Duniani kunasikika vilio vya aina mbalimbali, mojawapo ya kilio kinachosika duniani NI KILIO CHA WAZAZI WAKILIA KWA KUWA WATOTO WAO HAWANA TABIA NJEMA.


Kila kukicha mmomonyoko wa maadili unakua kwa kasi; watoto wanapiga wazazi, wanaua wazazi n.k imefika hatua wazazi wengine wanajuta kuzaa, wengine wamesema "ni heri kuwa tasa" - hayo maneno yanatokana na uchungu walionao wazazi.


MBINU ZA KUSHUGHULIKA NA TABIA KIBIBLIA

1. WAFUNDISHE WATOTO NENO LA MUNGU

(Kumbukumbu la torati 6:6-7)

--> Uwe na muda wa kuwafundisha watoto wako.

--> Wanunulie Biblia.

--> Wapeleke kwenye mafundisho.


2. CHAPA FIMBO PIA TOA MAONYO

(Mithali 29:15, 23:13-14, 22:15)

Watoto ambao hawajafikia utu uzima wanatakiwa kuchapwa viboko, watu wazima wape maonyo.


3. OMBEA MASIKIO YAZIBUKE

(Isaya 50:5)

-->Masikio yakizibuka watakuwa wasikivu.


4. WAPE MAUSIA

(Mithali sura ya 30, 31)

Chapisha Maoni

0 Maoni