(Warumi 12:16c)
"lakini MKUBALI kushughulishwa na MAMBO MANYONGE"
Kujishughulisha na mambo manyonge ni mojawapo ya jambo unalopaswa kufanya ikiwa unataka Mungu akuinue, akuamini na azidi kukutumia.
Kujishughulisha na mambo manyonge ni kufanya mambo yanayoonekana ni duni au mambo ya chini sana yasiyoendana na hadhi yako yaani ni kuiweka pembeni hadhi yako ili utimize jukumu fulani kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
BAADHI YA MAMBO MANYONGE
1. Kufagia au kudeki jengo la ibada.
2. Kufuta viti ili kuondoa vumbi.
3. Kumbebea mtumishi begi lake au kumbebea mtumishi Biblia anapopanda madhabahuni kuhubiri au kufundisha.
4. Kufua vitambaa vinavyotumika kupamba nyumba ya Mungu.
5. Kula na kukaa na watu wasio wa hadhi yako.
NB: Yesu aliwahi kufanya mambo yasiyoendana na hadhi yake; aliwahi kuwaosha miguu wanafunzi wake (Yohana 13:5-9), Yesu aliwahi kukaa na watoto, kama unavyojua watoto wana kelele n.k ndio maana mitume walitaka kuwazuia lakini Yesu alikaa nao (Marko 10:13-14)
0 Maoni