Faraja Gasto
(Waebrania 3:16-19)
Biblia inaripoti kuwa kilichosababisha waisraeli wengi kufia jangwani ni kutokuamini kwao sio jangwa.
Ukichunguza kwa makini safari ya waisraeli utagundua kuna roho chafu zilikuwa zikiwashambulia waisraeli ili kuhakikisha hawaingii kanaani baadhi ya roho hizo ni
1. roho ya kuchelewa.
2. roho ya kumsahau Mungu.
3. roho ya kutokuamini.
Kutokuamini ni kikwazo kikubwa cha kutopokea majibu na mambo mbalimbali kutoka kwa Mungu, kutokuamini ni kikwazo kikubwa cha kutotumiwa na Mungu, kutomsikia Mungu n.k
JINSI YA KUSHINDA TATIZO HILO
1. Fahamu na uamini Mungu hawezi kusema uongo.
(Hesabu 23:19)
--> Ukimuona Mungu ni muongo hautamuamini, hiki kiliwaponza waisraeli.
2. Tendea kazi neno la Mungu.
(Yakobo 1:22)
--> Mungu ni halisi na miujiza yake ni halisi kwa wanaolitenda neno lake (Isaya 55:11).
3. Fahamu na uamini Mungu anakuwazia mema.
(Yeremia 29:11)
--> Hata kama una magumu bado Mungu anakuwazia mema. Mungu ni mwema wakati wa shida na raha.
0 Maoni