MBINU ZA KIBIBLIA ZA KUMTAFUTA MUNGU


                       Faraja Gasto

(Isaya 55:6)

Wapo watu ambao wakisikia neno "kumtafuta Mungu" hujiuliza kama Mungu yuko ndani yangu namtafutaje? nawezaje kumtafuta Mungu?


Hayo ni baadhi ya maswali ambayo watu hujiuliza.


MAANA YA KUMTAFUTA MUNGU 

Ni kutenga muda kwa ajili ya kutaka kumsikiliza Mungu na kumuomba Mungu.


MBINU ZA KUMTAFUTA MUNGU

1. Kutenga muda kwa ajili ya kumuomba Mungu.

(2 Samweli 21:1) (Ezra 8:21-23) (Esta 4:15-17) 


2. Kutenga muda kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu kwa njia mbalimbali kama vile kusoma Biblia, kusoma vitabu vilivyoandikwa na watumishi wa Mungu, kusikiliza mafundisho ya neno la Mungu n.k

(Nehemia 8:1-9)(Wakolosai 3:16) (Yoshua 1:8)


3. Kuwaendea watumishi wa Mungu au kuwatafuta watumishi wa Mungu ili kutaka kusikia Mungu atakachokuambia kupitia wao.

(2 Wafalme 4:1-7) (2 Wafalme 5:9-10) (Matendo ya 10:7-8, 23-44)

-Waweza kuwaendea watumishi wa Mungu wakufundishe, wakushauri n.k kufanya hivyo ni kumtafuta Mungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni