Mbinu mojawapo ya kupima ukomavu wa kiuongozi (leadership maturity) ni KUANGALIA MWITIKIO WA KIONGOZI ANAPOPINGWA AMA KUKOSOLEWA (the way leader reacts after being opposed or criticized).
Ikiwa kiongozi atawachukia, atawashambulia, atawakandamiza au atatumia nguvu hasi kukabiliana na wapinzani ama wakosoaji wake basi hiyo ni ishara kuwa kiongozi hajakomaa kiuongozi.
(Ufunuo wa Yohana 12:7-9)
Ibilisi na wafuasi wake waliposhindwa vita kule mbinguni, MUNGU HAKUWANYANG'ANYA UWEZO WALIOKUWA NAO, MUNGU ALIWAACHIA UWEZO WALIOKUWA NAO. JAMBO HILO LINADHIHIRISHA KUWA MUNGU NI KIONGOZI HODARI TENA WA AJABU (EXCEPTIONAL LEADER).
NB: Kiongozi ambaye hajakomaa kiuongozi ni hatari kwa taifa, taasisi, jamii nakadhalika. Endelea kujifunza masomo ya uongozi kwenye Biblia.
0 Maoni