Faraja Gasto
Nguvu ndizo huamua mambo mbalimbali kama vile kiwango cha mafanikio, maendeleo, umbali nakadhalika.
Ili utembee umbali mrefu lazima uwe na nguvu zinazoendana na umbali huo, kwa mfano kama una gari halafu gari halina mafuta halitatoka lilipo, mafuta ndio yanaamua gari liende umbali gani, ukiweka lita kumi litakwenda umbali unaolingana na nguvu iliyomo.
Siri chache kuhusu nguvu
1. Huwezi kwenda umbali zaidi ya nguvu ulizonazo.
2. Huwezi kufanikiwa zaidi ya nguvu ulizonazo.
3. Huwezi kupata maendeleo zaidi ya nguvu ulizonazo.
4. Huwezi kumiliki na kutawala zaidi ya nguvu ulizonazo.
5. Huwezi kununua zaidi ya nguvu ulizonazo.
6. Huwezi kubeba chochote zaidi ya nguvu ulizonazo.
7. Huwezi kufaulu zaidi ya nguvu ulizonazo.
8. Huwezi kufanya jambo lolote zaidi ya nguvu ulizonazo.
Baadhi ya aina za nguvu
1. Maarifa.
2. Hekima.
3. Imani.
4. Afya.
5. Fedha na mali.
6. Watu.
7. Hamasa.
8. Upendo.
9. Furaha.
10. Uaminifu.
11. Uvumilivu.
12. Upole.
13. Amani.
0 Maoni