MAONO, NDOTO vs MAZINGIRA

 

                         Faraja Gasto

Baadhi ya mambo yanayotoka kwa Mungu ni ndoto na maono (Yoeli 2:28)


Kuna watu wana ndoto na maono lakini mazingira yanawakwamisha kutekeleza ndoto na maono yao.


Nitumie tafsiri ya mazingira inayojulikana sana "mazingira ni jumla ya mambo na vitu vyote vinavyomzunguka mwanadamu"


Mazingira ni kikwazo kimojawapo kinachosababisha watu wengi wasitekeleze ndoto na maono waliyonayo kwa kuwa shetani hutumia mazingira kuwakwamisha watu wasitekeleze ndoto na maono Mazingira ni kikwazo kimojawapo kinachosababisha watu wengi wasitekeleze ndoto na maono waliyonayo kwa kuwa shetani hutumia mazingira kuwakwamisha watu wasitekeleze ndoto na maono walionayo.


NINI UFANYE IKIWA MAZINGIRA NI KIKWAZO

Omba Roho wa Mungu ashughulikie mazingira yanayokukwamisha kutekeleza ndoto na maono aliyokupa Mungu.


(Matendo ya mitume 13:1-3)

Kuna kazi ambayo Mungu aliwaitia Barnaba na Sauli lakini mazingira yakawafanya wasiende kwenye kazi waliyoitiwa, ilibidi Roho wa Mungu aingilie kati kuwatoa ili waende kwenye kazi.


Roho wa Mungu anaweza kukutengenezea mazingira rafiki ili utekeleze ndoto na maono aliyokupa Mungu, OMBA.

Chapisha Maoni

0 Maoni