KULA UJANA vs KULIWA NA UJANA


                         Faraja Gasto

Ujana ni kipindi ambacho hakina tofauti na madawa ya kulevya kwa kuwa ni kipindi kinachosababisha vijana wengi kuharibikiwa.


Kipindi cha ujana ni kipindi kizuri kwa wanaotega masikio kusikia mashauri na maonyo ila ni kipindi kibaya kwa wasiotaka kupokea mashauri na maonyo.


Kuna matatizo ambayo hutengenezwa ujanani na athari zake huonekana ujanani wakati mwingine athari zake huonekana ukubwani (baada ya kupita kwenye ujana). Kwa mfano binti anaweza kufurahia ngono na utoaji mimba ila athari akaziona ukubwani na itamgharimu sana.


Jibu la vijana wengi ni "NAKULA UJANA AU ACHA NILE UJANA" pasipo kujua ujana hauliwi ila huwa unamla anayetaka kuula.


Kijana wa zamani alipogundua ujana ni kama madawa ya kulevya aliwapa vijana wosia kwa kusema "MKUMBUKE MUUMBA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO" (Mhubiri 12:1a)


Kwa hiyo ukitaka ujana usikuathiri fanya hivi

1. Fanyika mwana wa Mungu kwa kumwamini Yesu (Yohana 1:12-13)


2. Ishi kwa kufuata maelekezo ya neno la Mungu (Zaburi 119:9

Chapisha Maoni

0 Maoni