KUWA NA BUSARA KAMA NYOKA NA KUWA MPOLE KAMA NJIWA


                       Faraja Gasto

(Mathayo 10:16)


Ili uweze kuelewa maana ya Yesu Katika andiko hilo ni muhimu sana kuzifahamu tabia za nyoka na njiwa.


Nyoka ni mnyama mwerevu na njiwa ni ndege mpole, upole maana yake ni kutotaka makuu au kutotaka migogoro.


Kwa nini uwe mwerevu kama nyoka ni kwa sababu ya usalama wako, kuna wakati Katika kushuhudia au kueleza habari za Yesu unaweza kuinukiwa ikitokea umeanza kuona dalili za kuinukiwa wewe ondoka hapo kwa usalama wako Kwa kuwa Yesu hakututuma kupigana bali kufikisha habari njema.


(Yohana 8:58-59)

Kuna wakati Yesu alikuwa akihibiri ghafla watu wakainuka wakataka kumpiga mawe YESU AKAJIFICHA, hiyo ndio maana mojawapo ya kuwa na busara kama nyoka. Nyoka anapoona hatari huwa anajificha.


Kwa nini uwe mpole kama njiwa, njiwa huwa hataki makuu hataki migogoro anapoona Kuna hali ya hatari huamua kutulia au kuondoka mahali pa hatari.

Katika kushuhudia Kuna wakati unaweza kukutana na maswali ya kipuuzi, watu kukudharau nakadhalika tena unaweza kudharauliwa na mtu unayemzidi cheo, elimu, uwezo wa kiuchumi nakadhalika inapotokea hali kama hiyo wewe kuwa mpole usitake makuu, usianze kujibu mapigo Kwa kuwa Yesu hakututuma kujibu mapigo bali kupeleka habari njema.

Chapisha Maoni

0 Maoni