FUNDISHO KUU NA AMRI KUU KATIKA BIBLIA


 

Fundisho kuu katika Biblia sio kunena Kwa lugha, sio kupanda mbegu, sio kuyatabiria maisha yako, sio kufanikiwa kiuchumi, sio kupata watoto mapacha, sio kupata mke mwenye umbo namba nane, sio kupata mume mwenye sex body, sio kujua namna ya kumkomoa shetani,  sio kupata mipenyo nakadhalika.


FUNDISHO KUU KATIKA BIBLIA NI UPENDO (LOVE) PIA AMRI KUU NI UPENDO (LOVE) (MATHAYO 22:37-40).


Upendo ndio kila kitu Katika maisha ya kiroho na kimwili, Mtume Paulo alipogundua Siri hii alisema "nijaponena Kwa lugha za wanadamu na Malaika, nijapokuwa na mafunuo, nijapofanya chochote nje na upendo ni bure tu (1 WAKORINTHO 13:1-8)


Upendo ni elimu ambayo unaweza kujifunza katika Biblia, ni elimu inayoweza kubadilisha maisha yako ya kimwili na kiroho.


Upendo ndio silaha hatari kuliko silaha yoyote unayoijua (eeee sijakosea upendo ndio silaha hatari kuliko silaha yoyote unayoijua)


Upendo ndio nguvu inayoweza kuleta mabadiliko makubwa Katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu.


😍😍😍😍😍😍😍😍😍😍😍😍😍😍

Chapisha Maoni

0 Maoni