(Waebrania 13:1)
Lengo la somo: ni namna tunavyoweza kudumisha upendano wa ndugu katika Kristo Yesu.
UTANGULIZI
Sisi sote tuliomwamini Yesu bila kujali madhehebu yetu tumefanyika kuwa ndugu tena ni ndugu wa damu kwa kuwa tulikombolewa kwa damu ya Yesu (Ufunuo wa Yohana 5:9)
Hivyo tunapaswa kudumu katika upendo.
NAMNA YA KUDUMISHA UPENDANO
1. Kusameheana
(Wakolosai 3:12-13)
-->Kupendana ni pamoja na kusameheana.
2. Kujuliana hali na kutembeleana
(Kutoka 2:11-12)
-->Wajulie hali ndugu zako kwa njia ya simu, kuwatembelea n.k.
3. Kuombeana
(Waefeso 6:18)
-->Tunapaswa kuombeana ajili ya mambo mbalimbali.
4. Kumuona mwenzio kuwa ni bora kuliko nafsi yako
(Wafilipi 2:3-4)
--> Tatizo la mwenzako lichukulie kuwa ni la kwako.
5. Kutumia vema ndimi zetu
(Wakolosai 4:6)
-->Tutumie ndimi zetu kujengana sio kujeruhiana.
HITIMISHO
Kupendana ni amri ya Bwana Yesu (Yohana 15:12)(1 Yohana 3:11) lazima tupendane.
0 Maoni