KUMWENDEA MUNGU KWA FARAGHA

                       Faraja Gasto

Kumwendea Mungu kwa faragha
1. Ni kuwa na muda binafsi wa kumuuliza Mungu, kumuomba Mungu, kumsifu na kumuabudu na kujifunza neno la Mungu.


2. Kujitenga na watu ili kumwendea Mungu kibinafsi.


Mbinu mojawapo iliyowasaidia wanafunzi wa Yesu kufahamu siri nyingi na kufahamu mengi NI KUMWENDEA YESU KWA FARAGHA (Mathayo 24:3-44)(Marko 4:10-33)


Mbinu mojawapo iliyomsaidia BWANA YESU kufanikiwa katika huduma alipokuwa duniani NI KUMWENDEA MUNGU BABA KWA FARAGHA (Mathayo 14:13)(Mathayo 17:1-7)(Mathayo 17:36)


FAIDA CHACHE ZA KUMWENDEA MUNGU KWA FARAGHA
1. Utafunuliwa (utapata ufunuo kutoka kwa Mungu)
- Zipo mbinu mbalimbali za kupata ufunuo kutoka kwa Mungu, mbinu mojawapo ni kumwendea Mungu kwa faragha.
-Kitabu cha ufunuo wa Yohana, Yohana alifunuliwa alipokuwa faraghani kwenye kisiwa cha Patmo (Ufunuo wa Yohana 1:9-20).


2. Utapata maelekezo au miongozo kutoka kwa Mungu.
(Kutoka 19:3-25)


3. Utajua usiyoyajua.
(Yohana 3:1-21)(1 Samweli 21:1)

Chapisha Maoni

0 Maoni