Faraja Gasto
Upandaji wa makanisa ni nini?
1. Ni kuanzisha kanisa mahali ambapo hakuna kanisa.
2. Ni kuanzisha taasisi ya kutoa huduma za kiroho na kijamii kwa misingi ya neno la Mungu (Biblia).
3. Ni kuanzisha kanisa mahali ambapo kuna makanisa machache ili kuwasogezea wanadamu huduma za kiroho ili kuwaepushia watu adha ya kwenda mbali kupata huduma za kiroho.
4. Ni kuanzisha ngome ya kushughulikia kazi za shetani.
AINA ZA UPANDAJI KWA MAKANISA
1. Kupanda kanisa kwa kuitwa na Mungu.
2. Kupanda kanisa kwa kutumwa na dhehebu.
3. Kupanda kanisa kwa sababu binafsi.
- Kuanzisha kanisa kutokana na kiburi cha kutotaka kuchungwa, tamaa, kuiga nakadhalika.
KWA NINI MUNGU ANATAKA MAKANISA YAANZISHWE?
Hizi ni sababu chache;
1. Mungu anawapenda wanadamu (Yohana 3:16)
2. Mungu anataka wanadamu wawe na ushirika naye.
- Ndio maana Mungu anataka kuona watu wakimwabudu, watu wawe na eneo la kukutania ili kuimarisha ushirika na Mungu (Matendo ya mitume 2:41-42,44-47)
3. Mungu anataka makanisa yaanzishwe kwa kuwa WATU WANATESWA NA SHETANI, kanisa ni ngome ya Mungu ya kushughulikia kazi za shetani (Matendo ya mitume 16:16-18)
4. Mungu anataka watu wamjue, kanisa ndio taasisi inayomfunua Mungu (Mathayo 28:19-20)
KANUNI KADHAA ZA KIBIBLIA ZA UPANDAJI WA MAKANISA
1. Uinjilisti au ushuhudiaji.
(Matendo ya mitume 2:40-47)
2. Kuwa na mahali pa kukutania.
(Matendo ya mitume 2:46)(Matendo ya mitume 16:16a)(Filemoni 1:2)
- Kanisa linaweza kuanza kwenye nyumba ya anayeanzisha kanisa, kwenye nyumba ya mtu aliyejitolea kanisa lianzie kwake, kwenye ukumbi, kwenye darasa au kwenye jengo lililojengwa kwa ajili ya kanisa.
3. Kukubali kulipa gharama.
(Luka 14:27)
- Kupanda kanisa kutagharimu muda, nguvu za mwili, fedha nakadhalika.
Mungu akubariki kwa hayo machache.
0 Maoni