KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU HAITAFANIKIWA


                         Faraja Gasto


(Isaya 54:15-17)


Shida mojawapo waliyonayo watu wengi NI KUTOLIAMINI NENO LA MUNGU KAMA LILIVYO.


Biblia inaposema "kila SILAHA itakayofanyika juu yako haitafanikiwa" inamaanisha silaha yoyote kama vile bomu, risasi, mkuki, simu, asidi, mshale, uchawi, kisu, moto, panga na silaha yoyote unayoifahamu.


Ukianza kuliamini neno la Mungu kama lilivyo utashangaa yatakayokuwa yanatokea, utashangaa silaha inakuwa haina uwezo juu yako na neno hilo la silaha yoyote haitafanikiwa linaanza kuwa halisi kwako.


Soma mifano hii michache iimiarishe Imani yako juu ulinzi wa Mungu

1. Moto haukuwateketekeza wakina Shadraka, Meshaki na Abednego Kwa kuwa waliamini Mungu wao anaweza kuwaokoa na ule moto (Danieli 3:16-28)


2. Sumu ya nyoka haikumuua Mtume Paulo (Matendo ya mitume 28:3-6)


3. Ukiamini hata ikitokea umenyweshwa kitu cha kufisha hakitakudhuru (Marko 16:18)


4. Uchawi hautakudhuru (Hesabu 23:23)

Chapisha Maoni

0 Maoni