Bahati
mbaya ni kwamba waimbaji wengi sio waombaji, wanapenda kuimba halafu hawataki
kuomba, wanapenda kuimba madhabahuni halafu hawataki kuwa na mahusiano na Mungu
mwenye madhabahu.
Waimbaji
wengi hawana mafunuo kwa kuwa ni waimbaji wasio waombaji ndio maana imekuwa si
ajabu kuwasikia wakibadili nyimbo za wasanii wanaoimba upumbavu halafu
wanaziita nyimbo za injili.
Ni
vema kila muimbaji afahamu kuwa utumishi ndani ya Yesu Kristo unaongozwa na
Roho Mtakatifu, kama ukimsukumia mbali Roho Mtakatifu utabaki unajiita muimbaji
wa nyimbo za injili halafu injili unayoihubiri haina mguso wowote.
Kuna
waimbaji wamefariki lakini nyimbo zao bado zina mguso japo wao hawapo.
Ili
uimbaji wako uwe na maana, unganisha vitu viwili UIMBAJI NA UOMBAJI.
0 Maoni