Faraja Gasto


Yamkini unatamani kuona msimu mpya kwa ajili yako binafsi, familia, ukoo, mtaa, kijiji, mkoa, nchi n.k


Zifuatazo ni baadhi ya mbinu za kibiblia za kufungua misimu mipya;-

1. TOBA

(Matendo ya mitume 3:19)

Mtume Petro aliwaambia watu "TUBUNI basi mrejee ili dhambi zenu zifutwe ZIPATE KUJA NYAKATI za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana"


- Toba inaweza kufungua msimu mpya kwa mtu binafsi, nchi n.k


(Luka 15:17-24)

Mwana mpotevu alipotubu msimu mpya ukaja kwenye maisha yake.


2. SADAKA

(Mwanzo 8:20-21)

Sadaka alizotoa Nuhu zilifungua msimu mpya kwa dunia yote.


(1 Wafalme 3:4-14)

Sadaka alizotoa Mfalme Sulemani zifungua msimu mpya kwa ajili yake na taifa lake.


3. MAOMBI HUSUSANI MAOMBI YA KUFUNGA

(Esta 4:16)(Esta 8:1-17)

Maombi ya kufunga yalifungua msimu mpya kwa wayahudi.


(2 Mambo ya nyakati 7:14)

Maombi yanaweza kufungua misimu mipya.