NAMNA YA KUTENGENEZA FIKIRA ZA UJASIRIAMALI

Faraja Gasto
+255767955334
Utangulizi
Wajasiriamali karibia wote wanakumbana na changamoto mbalimbali.
Mojawapo ya changamoto kubwa inayowakabili ni KUKOSA FIKIRA ZA UJASIRIAMALI
Fikira za ujasiriamali ni pamoja na:-
v  Namna ya kuanza biashara
v  Namna ya kupata mtaji
v  Namna ya kufahamu fursa
v  Namna ya kutatua changamoto katika ujasiriamali
v  Namna ya kutanua soko
N.K

Ujasirimali ni nini? (Tafsiri yangu)
Ni kulifanya wazo au ujuzi ulionao au taaluma au kipaji ulichonacho viwe biashara halisi (biashara inayoonekana).

Mjasiriamali ni nani? (Tafsiri yangu)
Ni mtu ambaye amelifanya wazo la biashara alilonalo au taaluma aliyonayo au kipaji alichonacho au ujuzi alionao uwe biashara halisi (biashara inayoonekana).

Namna ya kutengeneza fikira za ujasiriamali
1.Badilishana mawazo na wajasiriamali wengine
-Kubadilishana mawazo kutakusaidia
(a).Kupata mawazo ya biashara
(b).Kuelewa soko limekaaje na wewe uingieje
(c). Kupata uzoefu mpya
(d).Kufahamu changamoto za aina hiyo ya ujasirimali
N.K

2.Fuatilia taarifa za kibiashara katika redio, televisheni, mtandao  au kwa njia ya kusoma vitabu, makala n.k
Taarifa ni aina mojawapo ya rasilimali ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwa nayo.
-Taarifa zitakusaidia kufahamu:-
(a).Uhitaji wa watu wa eneo fulani
(b).Fursa zinazopatikana eneo fulani
(c).Kufahamu bei za bidhaa
N.K

3.Waza namna ya kutatua tatizo la kihuduma katika eneo fulani
-Kwa mfano kama watu wanafuata bidhaa fulani mbali, wewe waza namna ya kuwaletea hiyo bidhaa karibu yao.
Kwa mfano msiba ni jambo lisilopendwa kwa kuwa ni jambo la huzuni lakini kwenye misiba huwa kuna fursa mbalimbali, kwa mfano ukitokea msiba lazima watu watakusanyika kwa hiyo watahitaji turabai za kuweka juu kwa ajili ya kupata kivuli pia kuna watu huwa wanalala kwenye misiba usiku, wakati mwingine wanahitaji turubai za kulalia kwa hiyo kama una turubai unaweza kuwakodishia maana hiyo ni biashara, wakati unaomboleza pamoja nao unatumia hiyo fursa kufanya biashara.
Ninakumbuka wakati nikiwa chuoni, tulikuwa tunafanya makongamano mbalimbali ya kidini tulikuwa tunahitaji vyombo vya muziki vya kukodi na vyombo vya chakula vya kukodi, ninachotaka uone hapa hata vyuoni kuna fursa, kwa sababu watu waliokuwa na vyombo tulikuwa tunawalipa pesa wanatukodishia vyombo.
Ndio maana nakuambia waza namna ya kutatua tatizo la kihuduma katika eneo fulani.

4.Hudhuria semina, warsha, na matamasha ya ujasiriamali
-Unapohudhuria kwenye semina, warsha au matamasha utakutana na shuhuda za watu waliofanikiwa katika biashara fulani, itakusaidia kujua walianzaje, walikabiliana vipi na changamoto, pia utajipatia ufahamu wa kutosha utakaokusaidia katika ujasiriamali.

Chapisha Maoni

0 Maoni