Hisa ni nini?
Wengi miongoni mwetu
wamekuwa wakitaka kujua HISA ni nini, shauku hii imenifanya nidodose kidogo juu
ya hisa kwa faida ya wengi. Kwa tafsiri lahisi HISA NI UMILIKI.
Mtu akisema nina hisa
NMB anamaanisha ana miliki NMB. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati
wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida inayopatikana katika kampuni).
Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na
hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake.
Mfano- Kampuni yaweza
kuwa na hisa 1000, ikaamua kuuza hisa 500 na hisa 500 zikabaki akiba. Wale
watakaonunua hizo hisa 500 , wanakuwa wametoa mtaji kwa kampuni na kwa maana
hiyo ndio wamiliki. Mwenye kuweza kununua hisa 251 atakuwa amenunua hisa nyingi
zaidi kuliko yeyote na anakuwa na nguvu ya maamuzi katika vikao na gawio
atapata kubwa kwa sababu ndie aliechangia mtaji mkubwa.
Faida
za kuwa na hisa:
1. Unapata fursa ya
kuwa mmoja ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ama moja kwa moja au kwa
kuwakilishwa.
2. Mwanahisa
anapofariki shughuli za kampuni haziwezi kuyumba kwa sababu jukumu la kazi za
kila siku lipo mikononi mwa menejimenti
3. Ni lahisi zaidi kuuza
HISA pindi unapoona hauhitaji kuendelea na umiliki
4. HISA ni dhamana
(badala ya kuweka nyumba/shamba ili uweze kukopeshwa na taasisi za fedha waweza
kuweka dhamana ya hisa zako)
5. Kampuni inapofanya
vizuri sokoni ama kwa kutoa huduma/bidhaa bora au kwa kuwa na mipango mkakati
mizuri thamani ya HISA hupanda. Wapo walionunua hisa za NMB tshs 600 lakini leo
ni zaidi ya tshs 950.
Kwa maana hiyo mbali
ya gawio mtu anaweza kuuza hisa kwa bei inayomlipa akilinganisha na bei ya
kununulia.
JINSI YA KUNUFAIKA NA
SOKO LA HISA
1. Nimeona leo
nishare na nyinyi kuhusu soko la hisa na jinsi ya kunufaika nalo.Kwa kifupi
kuwa na hisa ni kumiliki sehemu ya kampuni au kuwa mmiliki wa kampuni hiyo kwa
maana hiyo unakuwa na nafasi ya kushiriki kufanya maamuzi ,kupata faida au
hasara katika kampuni hiyo.
Unanunuaje Hisa?
Hisa katika soko la
hisa dare s salaam huuzwa na brokers kama orbit securities, na wengineo wapo
wengi tu ila hawa ndio ninawafahamu. Unaweza pata taarifa zaidi kupitia website
ya soko la hisa la dare s salaam www.dse.co.tz.
Faida za kununua
hisa;
i) Hisa hukuwezesha
kupata gawio la faida ya kampuni hiyo ikiwa itatangaza faida .
ii) Ukiwa na
mwanahisa unaweza kutumia cheti cha hisa (share certificate) kuombea mkopo,
ingawa hili ni jambo geni kwa Tanzania .
iii) Hukulinda dhidi
ya anguko la thamani ya fedha kwa kuwa fedha huwa na tabia ya kupoteza thamani
unaponunua hisa inaweza kukulinda kwa kuwa hisa huwa na tabia ya kupanda
thamani kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa.
iv) Unaweza nunua na
kuziuza wakati wowote.
Jinsi ya kununua hisa
kwa kampuni unayohitaji;
Unapofika kwenye soko
la hisa la dare s salaam kuna makampuni mengi yaliyoorodheshwa kuuza hisa zao
mfano CRDB, NMB, USL, DCB, KCB, SWISS PORT, TBL, TTP na nyingine nyingi.
Sasa ni kampuni ipi
ununue hisa ni vyema ukaangalia mambo yafuatayo;
i) Performance ya
kampuni. Mfano kampuni kama inafanya kazi vizuri kwa weledi na inamategemeo ya
ukuaji wa kampuni hiyo kama kutanua matawi, kuongeza product au kukua kwa
biashara katika kampuni hiyo basi hiyo ni kampuni nzuri mfano.
Ukisikia kampuni
imetanua soko lake kama CRDB ilivyofungua matawi nchi za nje inamaana ya kuwa
faida ya kampuni hiyo itaongezeka na hivyo gawio linaweza kuwa kubwa na wewe
kupata faida na pia bei ya hisa itaweza kuongezeka hivyo utapata faida pia
pindi ukiamua uza hisa zako.
ii) Bei ya hisa na
uimara wake (stable share price) kuna kampuni ambazo bei zao za hisa wakati
wote ni nzuri kwa maana hazishuki sana au mara kwa mara na pia zina tabia za
kuongezeka mfano TBL , SWISS PORT, TCC.
iii) Wakati wa
kununua hisa . ni muhimu pia kuangalia ni wakati gani unanunua hisa mfano.
Wakati ambao hisa ndio zinaingizwa au kuuzwa kwa mara ya kwanza kwenye soko la
hisa bei huwa ni ndogo sana na baada ya hapo mara nyingi bei huongezeka ingawa
kuna wakati hushuka pia .
Lakini bei ya hisa
hupanda kushuka kutokana na nyakati katika mwaka mfano ifikapo mwishoni mwa
mwaka na mwanzoni mwa mwaka bei hushuka na kuwa ndogo zaidi ila katikati ya
mwaka bei huanza kupanda kwa kasi kubwa zaidi
iv) Uwepo wa taarifa
nzuri katika Sekta iliyo kampuni hiyo au katika kampuni hiyo. Mfano imekuwa
ikisikika kuwa benki ya CRDB itakuwa inatumika kulipia mishahara ya baadhi ya
wafanyakazi wa serikali basi siku ukisikia imeingia mkataba huo au imeanza kutumika
kulipia mishahara hiyo basi nenda kanunue hisa hizo haraka kwani bei ya hisa
itaanza kupanda na pia gawio la faida litakuwa kubwa.
Mfano mwingine ni kwa
kampuni ya SWISS PORT kampuni hii inadeal na mizigo kwenye viwanja vya
ndege,nafikiri taarifa ya kutanuliwa kwa uwanja wa ndege ya Dare s salaam
inafahamika hivyo ni wakati mzuri kununua hisa wakati huu kwani pindi uwanja
utakapokamilika basi kampuni itakuwa na biashara kubwa bei ya hisa itaongezeka
na faida pia
v) Wingi wa makampuni
katika soko la hisa. Mfano kuna mabenki zaidi ya matano hii inamaana benki hizi
zinagombea wateja hii ni kwa wateja wote wale wanaowahudumia na wale wa kwenye
soko la hisa hivyo bidhaa zao zipo za kutosha na bei itakuwa ya kawaida mambo
ya demand na supply. Kwa bei ya leo kampuni inayoongoza ni TCC- 17000, TBL
15000, JHL 10620, SWISS 6600,ACA-6540. Makampuni haya yote yanafanya shughuli
tofauti na bei zake ni nzuri zaidi.
Jinsi ya kujua faida
kuna namna mbili kupitia dividend/gawiwo na capital gain sijui kiswahili
tunaiitaje! Faida kupitia gawiwo unalipata pale kwa mfano unamiliki hisa 5000
then Co. Ikatangaza kwenye kila hisa 1 utapata gawiwo la sh.100 then hapo
utapata faida ya(5000×100)= sh.500,000# mkuu na Capital gain ni pale kwa mfano
ulinunua kila hisa 1 kwa sh.500 na unahisa 5000 then ulitumia(500×5000)=
sh.2,500,000 kama mtaji wako so ikitokea leo ukauza hisa zako na kila hisa
ukauza kwa sh.1000 manake itakua ni 1000×5000(idadI ya hisa unazomiliki)=5,000,000
then faida yako hapo ni ile pesa uliyopata kipind umeuza hisa zako 5,000,000
kutoa pesa ulizonunulia hisa zako 2,500,000=2,500 000 pole kwa maelezo marefu
mkuu wangu!!
HASARA ZA HISA
1. Hasara ni pale
unapokuwa na hisa chache kwani unakuwa kama unasindikiza wengine. Gawio unapata
dogo na unakuwa huna ushawishi katika maamuzi. Hasara nyingine ni pale kampuni
inapofanya vibaya, thamani ya hisa hupungua, waweza nunua hisa 1 kwa tsh 1000
ukauza 500 au hela zako zikazama. Ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya
kununua HISA
2. Ni kwa nini HISA
za CRDB zilishuka thamani?
Nitachangia kidogo...
Kwanza
kabisa,ningependa pia kusema kuwa hisa, zikiwa kama sehemu ya umiliki wa
kampuni, soko lake ni kama la bidhaa nyingine yeyote..mtu atakubaliana na mimi
kuwa kuna sababu zaidi ya moja inayoweza kupelekea kupanda au kushuka kwa bei
ya bidhaa fulani sokoni wakati fulani.
Inaweza kuwa ni
sababu ya kupungua/kufurika kwa bidhaa husika sokoni, kuwepo kwa bidhaa
shindani bora zaidi, hisia ya wateja kuhusu kukosekana kwa bidhaa hiyo hapo
baadaye na hivyo kutaka kununua kiasi kikubwa leo na kadhalika....
Primarily,ni kwamba
bei ya hisa sokoni inakuwa determined solely na demand vs supply ya hisa at a
time ni kweli kabisa. Lakini je, ni nini kinachopelekea mtu kutaka kuuza au
kununua hizo hisa na hivyo kuathiri kiasi hicho cha demand/supply ya hisa
sokoni at a time? Sababu ni nyingi..mfano:
1) Current company
profits - Kuna watu wanaodhani kuwa kampuni ikipata faida kubwa mwaka huu
kuliko uliopita basi itakuwa inafanya vizuri na hivyo wanaamua kuwa sehemu ya
wamiliki na hivyo kutaka kununua hisa zake. Hata hivyo faida ya sasa ya kampuni
inaweza isiwe kipimo tosha cha uzuri au ubaya wa kampuni.
Mfano, kwenye hii
case ya CRDB, inawezekana faida yake kubwa imetokana na vyanzo visivyoweza
kujirudia mwakani (one - off transactions) kama kuuzwa kwa baadhi ya assets
zake n.k..mwekezaji anapoona kuwa kampuni imeshindwa kutengeneza faida kwenye
ile biashara yake kuu, basi ataona kuwa uwezo wa kampuni kutengeneza faida
utakuwa mdogo pia huko miaka ya mbele na hivyo kutaka kuuza hisa zake.
2) Company
prospects/Investment plans (Mipango endelevu) - Kampuni inaweza kutengeneza
faida nzuri leo, lakini kwa kulinganisha mipango mikakati yake ya muda mrefu,
faida yake haitaongezeka kwa kasi kama ile ya washindani wake wa karibu. Kwa
matarajio ya kupata faida zaidi baadaye, mwekezaji anaweza kuamua kuuza hisa
zake na kununua za kampuni nyingine yenye mipango yenye faida zaidi huko
mbeleni.
3) Decline in
company's market share - Wawekezaji siku zote hutaka kuweka pesa zao pale
ambapo wanahisi zitakuwa na faida kubwa zaidi. Kampuni inaweza kuwa imepata
faida leo, lakini ukubwa/umahiri wake kwenye soko lake la bidhaa ukawa
unapungua taratibu. Hivyo wawekezaji wataona uwezekano wa kutengeneza faida
zaidi ikiwa watawekeza kwenye hiyo kampuni nyingine inayoonyesha ukuaji wa soko
lake la bidhaa ingawa hapa walipowekeza sasa kumepatikana faida pia.
4) Temporary
buyers/sellers - Masoko ya hisa duniani kote siku hizi yametawaliwa na watu
wanaotaka kununua hisa na kukaa nazo kwa muda mfupi tu mpaka hapo bei
itakapopanda kidogo ili wauze wapate faida, halafu wanunue nyingine na kuuza
tena kwa mtindo huo huo. Hii inaweza kuwa kweli kwa case ya CRDB pia.
Kwamba hawa
wawekezaji waliopeleka sokoni walikuwa wanasubiria kampuni itangaze gawio la
faida kwa mwaka (dividends), wachukue faida yao halafu wauze hisa zao na
kupeleka sehemu nyingine. Utashangaa kuwa kuna watu huwa wanawekeza ada za
shule za watoto wao kwenye hisa na wakati wa kulipa ada ukifika inabidi tu
wauze ili walipe ada..no matter what!
5) Wawekezaji kulipa
mikopo - hii hutokea mara nyingi wakati kampuni nzuri ikiingiza hisa zake
sokoni kwa mara ya kwanza. Wawekezaji huweza kuchukua mikopo benki, kununua
hisa na kukaa nazo, na kuziuza pindi bei inapopanda sokoni (au wakati wowote
muda wa kurejesha mikopo hiyo benki unapofika, bila kujali bei ya hisa sokoni
wakati huo!)
6) Speculative buyers
(wanunuzi watabiri) - Hawa ndio wameshamiri kwenye masoko ya hisa duniani kote,
na ndio chanzo kikuu cha financial crisis iliyoikumba Marekani miaka ya juzi.
Ni kwamba badala ya watu kununua hisa za kampuni kwa sababu ya uwezo wake wa
uzalishaji wa sasa hivi, ununuzi wa hisa unakuwa umeegemea zaidi kwenye
yatakayotokea kwenye kampuni miaka hata 20 au 100 ijayo.
Kunakuwa na watu
wapiga debe, wanaochimba (au kupika) habari za mipango ya kampuni (au ya
serikali, itakayoneemesha mapato ya kampuni) hata miaka 10 huko inayokuja. Kwa
hivyo basi watu hawa kwa maneno yao wanaishia kusababisha bei ya hisa
kuongezeka ama kupungua...
kwa hivyo kwa kujibu
swali lako dada Ashadii, kutokana na kuwepo hasa hasa kwa wanunuzi/wauzaji wa
hisa wa category namba sita (6) hapo juu, mara nyingi bei ya hisa sokoni
haiendani moja kwa moja na ubora wa kampuni kwenye kuzalisha fedha kwa sasa.
Kifupi kuna mambo
meengi tu yanayoweza kufanya prospective investors wakaongeza ama kupunguza
imani yao kwa kampuni fulani. Ndiyo maana unaweza kuona wakati mtu kama Steve
Jobs alipokuwa anakaribia kujiuzulu kama Apple CEO ilibidi kufanyike marketing
campaign ya kutosha ku-restore investor confidence na kuwadhihirishia watu kuwa
kampuni itaendelea kuwa kwenye mikono salama, itaendelea kupata faida, na hivyo
watu hawana haja ya kuuza hisa zao kwa hofu ya kupata hasara huko mbeleni.
In a nutshell, the
best way to buy or sell shares is to just act like a smart layman, huhitaji
technicalities nyiingi kuhusu sijui faida ama hasara ya kampuni leo, earnings
per share, etc...angalia mifano ya maswali anayotakiwa kujiuliza layman hapa:
(a) Twiga/Simba
Cement zinazalisha cement? Je cement itaendelea kuwa bidhaa inayohitajika na
watu wengi? Je demand yake ni kubwa? Je bidhaa za kampuni zina ushindani mkubwa
sokoni? Je kampuni ina uongozi mzuri? kama majibu ni ndiyo badi nunua
hisa..lakini mwaka 2014 ukishasikia Dangote Cement imeanza kuzalisha cement
kule mtwara kwa kiwango kinachotosheleza demand ya Afrika Mashariki yote,,,you
should know it is a sign that Twiga's share of the cement market is about to
decline and..may be, may be you need to sell your shares!
(b) Hisa za Precision
Air...ilikuwa ni sahihi kabisa kwa watu kununua hisa za Precision Air wakati
ambapo kampuni ilikuwa inaoperate kama monopoly, bila mshindani. Hii ni kwa
sababu lazima kampuni ingetengeneza pesa tu, iwe isiwe (walau ikiwa na uongozi
makini kidogo).
Lakini je, baada ya
kuja kwa fast jet, Precision ina uwezo wa kuendelea kutengeneza pesa? Je ina
uwezo/mipango gani ya kupambana na hii bei ndogo ya mshindani wake ilhali wote
tunajua wateja wanavyopenda kulipa gharama ndogo kuliko kubwa?..haya ni maamuzi
ambayo yanaweza kufanywa na a smart layman...trust me,hayo ni muhimu kuliko
expert advice...
Nyongeza kutoka kwa
Mwl.Faraja Gasto
Kabla ya kuwekeza ni
muhimu kupata ushauri kutoka kwa Mungu maana ndiye anayefahamu yaliyopita,
yaliyopo na yajayo.
0 Maoni