Faraja Gasto
+255767955334
Mafanikio hayategemei kile ulichonacho(kazi, pesa, nafasi
uliyonayo, fursa unazoziona, watu n.k), mafanikio yanategemea JINSI UNAVYOTUMIA
KILE ULICHONACHO.
Unaweza ukaziona fursa nyingi kama haujui jinsi ya kuzitumia,
maisha yako hayawezi kubadilika.
Unaweza ukawa na kiwango fulani cha elimu (certificate
in.........., diploma in........, Bachelor degree in........, master
in.......... Phd, lld n.k) kama haujui jinsi ya kutumia elimu uliyonayo maisha
yako hayawezi kubadilika.
Unaweza ukawa na ukaribu na watu wenye uwezo wa kukusaidia ila
kama haujui jinsi ya kuwatumia, maisha yako hayawezi kubadilika.
Unaweza ukawa na nafasi fulani ila kama haujui kuitumia hiyo
nafasi, maisha yako hayawezi kubadilika.
Unaweza ukawa na kazi nzuri ila kama haujui kuitumia hiyo kazi,
maisha yako hayawezi kubadilika.
USISAHAU HILI
Shida waliyonayo watu wengi ni KUTOJUA NAMNA YA KUTUMIA VILE
WALIVYONAVYO na KUTUMIA VIBAYA VILE WALIVYONAVYO.
Narudia tena mafanikio hayategemei ulichonacho bali yanategema
jinsi unavyotumia ulichonacho.
2 Maoni
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFutaMkuu shukrani kwa ujumbe mzuri
JibuFuta