Faraja Gasto
+255767955334
Utangulizi
Katika makala hii ninapenda kufundisha watu
ambao tayari wana mitaji ya biashara, wako tayari kufanya biashara.
Yafuatayo ni mambo ya kufanya kabla
haujaanzisha biashara;-
1.Tathmini mazingira
unayotaka kuweka biashara yako ili ufahamu fursa zilizopo
Sio busara kuanzisha biashara ikiwa haufahamu
vema mazingira unayotaka kuweka biashara yako, usianzishe biashara maadamu una mtaji, anzisha baishara baada ya kufahamu
uhitaji wa watu katika eneo husika.
Ukianza kwa kutathmini mazingira ndipo utafahamu
fursa zilizopo katika eneo husika, utafahamu huduma gani au bidhaa gani
zinahitajika katika eneo husika.
2.Angalia
aina ya makazi yaliyopo
Ukitaka kujua hali za kipato za watu angalia
aina ya makazi wanayoishi, kwa mfano kama makazi yako karibu karibu na hakuna
uzio(fence) maana yake ni kwamba watu waishio kwenye eneo hilo wana kipato cha kawaida
au kipato cha chini.
Hii itakusaidia katika kupanga bei za bidhaa
zako au gharama za utoaji wa huduma.
3.Tafuta
kufahamu aina ya watu wa eneo husika
Kwa mfano kama eneo hilo lina waislamu wengi
uwe na uhakika ukianzisha biashara ya kuuza nguruwe haitakulipa, kama kuna
wasabato wengi uwe na uhakika biashara ya kuuza bidhaa zifuatazo haitakulipa;
biashara ya kuuza soda aina ya cocacola, biashara ya kuuza majani ya chai ya
kahawa n.k
4.Angalia
umbali uliopo kati ya makazi na huduma za jamii
Kwa mfano kama kuna maduka mawili hapo mtaani
na yanategemewa na mitaa mingine maana yake ni kwamba fursa ipo, ukiweka duka
utapata faida.
5.Fahamu
taratibu za kisheria ambazo unatakiwa kuzifuata kabla haujaanzisha baishara
Kwa mfano suala la leseni n.k
6.Fahamu
gharama zinazohusiana na biashara
Kwa mfano gharama za eneo la kufanyia
biashara, gharama za kumlipa mlinzi (kama utahitaji mlinzi), gharama za umeme
(kama utatumia umeme) na gharama zingine.
7.Tathmini
uwezo wako na kisha tumia fursa mojawapo kati ya zilizopo.
Baada ya kufanya tathmini kuhusu hayo mambo
matatu hapo juu ndipo utazame uwezo wako wa kiuchumi unakuruhusu kufanya
biashara gani katika eneo hilo.
0 Maoni