MUNGU ANATAKA UTAYARI WAKO
Mwl.Faraja Gasto
Bwana Yesu asifiwe!!!!
Watu wengi wanajitahidi kulikimbia kusudi la Mungu kwenye maisha yao kwa kuinua sababu(visingizio) na wengi wanadhani visingizio hivyo vitamfanya Mungu awaache waendelee kufanya wanayotaka.
Tabia hii ya kuinua sababu ili kulikwepa kusudi la Mungu ilianza zamani sana, wengine walimwambia Mungu kuwa umri wao hauruhusu kufanya kile ambacho Mungu anataka wafanye, wengine walidai umaskini walio nao unawafanya wasiwe tayari kutembea kwenye kusudi la Mungu, wengine walidai udhaifu wao unawafanya wasiwe tayari kutembea kwenye kusudi la Mungu LAKINI MUNGU HAKUONA KUWA HIZO NI SABABU ZA MSINGI
(Yeremia 1:4-7)(Waamuzi 6:14-15)(Kutoka 3:11, 4:10)
NATAKA NIONGEE NA WEWE
Yamkini na wewe unasema kuwa huwezi kumtumikia Mungu kwa kuwa hauna pesa, hauna elimu, haujui kingereza, hauna mavazi n.k
---Ni vema ufahamu kuwa hizo sababu sio za msingi mbele za Mungu, MUNGU ANATAKA UTAYARI WAKO TU WA KUTEMBEA KWENYE KUSUDI LAKE.
Fahamu fedha na dhahabu ni mali yake, lugha zimekuwepo kwa kuwa Mungu aliwagawia watu na hakuna aliyesomea lugha fulani, wanadamu walikuta wanajua kuongea lugha zinazosikika leo kwa hiyo kutojua lugha isiwe sababu, Udhaifu au ugonjwa sio sababu kwa kuwa Mungu aliyekuumba hajashindwa kukuponya na udhaifu huo au ugonjwa n.k
#Onyesha utayari umuone Mungu.
0 Maoni